Kuhusu Halmashauri ya Wiyala ya Meru

Wilaya ya Meru ipo Mashariki mwa mkoa wa Arusha na imelala kati ya latitudi 36 na Longitudi 37.Halmashauri inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kwa upande wa kaskazini na mashariki. Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa upande wa Magharibi na Kusini wilaya ya Simanjiro.

Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya Taifa ya watu na makazi ya mwaka 2002, Halmashauri ya Wilaya ya Meru inajumla ya wakazi 216,629. Aidha kwa mujibu wa kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni wastani wa asilimia 3.1 Halmashauri ya Wilaya ya Meru inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 280,879 Kati yao wanaume 140,108 sawa na asilimia 49.8 na wanawake 140,771 sawa na asilimia 50.2.Aidha Halmashauri inazo kaya 48,768 zenye wastani wa watu 5.

Utawala na Utumishi

Halmashauri ya wilaya ya Meru ki-utawala inazo Tarafa 3, kata 17 vijiji 71 na vitongoji 281 na jimbo moja la Uchaguzi la Arumeru mashariki lenye Waheshimiwa madiwani 17 wa kuchaguliwa,madiwani 6 viti maalumu pamoja na Mheshimiwa Mbuge.

ZABUNI

INVITATION FOR BIDS (IFB) BID No. LGA/001/2012/2013/W/06 & 07 (download the whole document here)

 INVITATION FOR BIDS (IFB) BID No. LGA/001/2012/2013/W/06 & 07 (download the whole document here)

MATUKIO


MATANGAZO

meridc_db

Login