Mkutano wa wananchi wa Usa-River wenye lengo la kuwashirikisha wananchi hao kwenye shughuli za maendeleo,hii ni baada ya Serikali kutoa fedha Kiasi cha Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha kituo cha Afya Usa-River kwa kufanya ukarabati pamoja na ujenzi wa majengo mapya 8 ambayo ni Jengo la upasuaji,Chumba cha kuhifadhia maiti,jengo la maabara,wodi ya akina mama,wodi ya watoto,nyumba ya mtumishi na kichomea taka,
Mkutano huu utafanyika leo tarehe 09 Desemba 2017 kwenye kiwanja cha mpira Ngarasero - Usa-River saa 8:00 mchana ambapo wananchi hao watachagua wawakilishi wao ,watakao wawakilisha katika uboreshaji wa kituo hicho cha Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 027 254-1112
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa