Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christoper J.Kazeri anawakumbusha wafanyabiashara kwenye Halmashauri hiyo kuwa msimu mpya wa kulipia leseni za vileo unaanza tarehe 01 mwezi Aprili 2018,hivyo wafanyabiashara husika wanatakiwa kulipia kwa wakati.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru kulipa kodi yaani Leseni za biashara na vileo kwa wakati kwani fedha hizo hutumika kuleta maendeleo kwenye Halmashauri hiyo kwakuwa hutumika kutekeleza shughuli za maendeleo.
"Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wafanyabiashara ambao watakutwa hawajalipia leseni za biashara wanazofanya " amesema Mkurugenzi Kazeri
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 027 254-1112
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa