IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
UTANGULIZI
Idara ya Usafi na Mazingira inatekeleza majukumu yake ya msingi kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serika mitaa (TAMISEMI). Huduma za masuala ya safi na Mazingira zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Usafi (Usimamizi wa Taka ngumu) na Mazingira inatekeleza majukumu yake ya msingi makuu mawili ambayo ni usafishaji wa Mji na Uhifadhi wa Mazingira.
USAFISHAJI (UDHIBITI TAKA NGUMU)
HIFADHI YA MAZINGIRA
SHERIA NA KANUNI ZINAZOIONGOZA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
Idara ya usafi na mazingira inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sera, sheria na kanuni zilizoanzishwa na kupitishwa na serikali.
Idara inatekeleza sheria tofauti katika majukumu yake ikiwa ni
WASHIRIKA (WADAU) KATIKA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
Idara ya usafi na mazingira inashirikiana na wadau mbali mbalimbali katika kutekeleza shughuli zake. Idara inashirikiana na shirika la hifadhi ya taifa ya Arusha (ANAPA) ili kuhakikisha uhifadhi wa mazingira katika Halmashauri ya Meru. ANAPA inatekeleza kusimamisha hifadhi hiyo ambayo ndio misitu mama na hifadhi ya wanyama pori katika Halmashauri ya Meru.
Vile ville idara inashirikiana na makampuni binafsi na vikundi vya kijamii katika kulindana mazingira, hii ikijumuisha upandaji wa miti, uhifadhi wa misitu na usafishaji wa mazingira. Miongoni mwa washirika na wadau hao ni GHECO Environment, MERU GREEN CLUB GROUP, OIKOS East Africa, Green Foundation, MALIHAI Club, DULUTI GREEN FOUNDATION TRUST, MOJIFA Environmental.
Shiriki eneo lako kuwa safi lipa ada ya gharama za uongoaji wa taka kwa mujibu wa sheria ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 027 297-482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa