Mradi huu umejumuisha shughuli za Ujenzi wa kidaka maji, Utandazaji wa bomba kuu na bomba za usambazaji Km. 10.846, Ujenzi wa vilula 27, Ujenzi wa tanki lenye ujazo wa mita 135 na Ujenzi wa matanki ya uvuaji maji ya mvua yenye ujazo wa lita 5,000, 3,000 na 2,000. Mradi huu umegharimu Tsh.296,920,362.02 hadi sasa zimelipwa Tsh. 183,096,266 bado Tsh. 113,824,096.02 zinahitajika kukamilisha malipo ya mkandarasi. Hata hivyo Mradi umekamilika kwa aslimia 100.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 027 297-482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa