Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Ndg Amani Mlay ametoa wito kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo kuondokana na hofu ya mlipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu badala yake wachukue tahadhari ya magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza Ofisini kwake ,Mlay amedhibitisha kutokuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye Halmashauri hiyo, na kueleza kuwa ,Mwanakijiji wa kijiji cha Mowara Kata ya Maruvango katika Halmashauri hiyo aliyehisiwa kuwa na dalili za kipindupindu wakati wa matibabu Wilayani Siha ambaye vipimo vilipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi amebainika kutokuwa na ugonjwa huo.
Aidha Mlay amewataka wananchi hao kuzingatia maswala ya usafi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Mlay ameeleza kuwa Halmashauri imekuwa ikitoa elimu ya Afya, kuhusiana na ujenzi na matumizi bora ya vyoo, kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula, kuchemsha maji ya kunywa ,kula vyakula vya moto , kuosha matunda kabla ya kula pamoja na kuweka safi mazingira yanayowazunguka kwa kutokutupa taka ovyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa