Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kipo kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Na. 9 ya mwaka 1982 Kifungu Na. 45 (1) (iliyorekebishwa mwaka 2000); Vile vile kazi na wajibu wa Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri zimeainishwa katika Memorandam ya fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2009(agizo No. 13 na 14).
Nia ya Ukaguzi ni kufuatilia rasilimali za serikali zinatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyotarajiwa kwa kuzingatia tija na ufanisi.
Malengo ya kufanya Ukaguzi wa Ndani ni kuwezesha kutoa uhakika(assurance) wa hali ya uendeshaji wa Halmashauri hasa kwa kuangalia vihatarishi ambavyo madhara yake ni makubwa katika mazingira ya Halmashauri; namna ya udhibiti wa vihatarishi vinavyohusiana na hatari ambazo zinaweza kuwa na athari katika kufikia malengo ya Halmashauri kuhudumia na kuleta maendeleo kwa Wananchi. Ukaguzi unatoa ushauri kwa Menejimenti juu ya mambo mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa shughuli za Halmashauri ili kuleta ufanisi.
Malengo ya jumla ya kitengo cha Ukaguzi wa ndani ni pamoja na:-
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa