Halmshauri ya Wilaya ya Meru ina jumla ya shule 143 za msingi na kati ya hizo 112 zinamilikiwa na serikali na 31 zinamilikiwa na Watu binafsi. Vilevile kuna jumla ya madarasa 101 ya Awali yanayomilikiwa na Serikali. Pia kuna Vituo vya Ufundi Stadi (VETA) vinne (Serikali vitatu na Binafsi kimoja), Vituo vya walimu (TCRS) vinne na Vituo vitano vya Elimu maalum.
Hamshauri ya Wilaya ya Meru kuna jumla ya shule za Sekondari 55 na kati ya hizo 29 zinamilikiwa na Serikali na 26 zinamilikiwa na Watu Binafsi. Kati ya shule za serikali tatu zina kidato cha tano ambazo ni Maji ya Chai, Kisimiri, na Makiba.
Ndani ya eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuna Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utoaji wa elimu ambapo baadhi ni Chuo Kikuu cha Makumira, Chuo Kikuu cha Arusha, Chuo cha Nelson Mandela, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Chuo cha Mifugo Tengeru, Kituo cha Kimataifa cha mafunzo ya Uongozi na Maendeleo –MS-TCDC (awali kilitwa Danish Centre).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa