VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA VILIVYOPO
Idara ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru in jumla ya vituo vya huduma 62 inajumuisha Hospitali 2 (1 ya serikali, 1 ya FBO) vituo vya Afya 9 (serikali 7 FBO 2) na zahanati 51( Serikali 27,FBO 13,Binafsi 9 na Taasisi 2)
|
GOVERNMENT
|
FBOs
|
PRIVATE
|
PARASTATAL
|
TOTAL
|
HOSPITAL
|
1
|
1
|
0
|
0
|
2
|
HEALTH CENTRE
|
7
|
2
|
0
|
0
|
9
|
DISPENSARIES
|
27
|
13
|
9
|
2
|
51
|
TOTAL
|
35
|
16
|
9
|
2
|
62
|
HUDUMA ZINAZOTOLEWA
Wagonjwa wan je (OPD)
Wagonjwa wanaolazwa (IPD)
Macho
Afya za Kinywa na Meno
Huduma za mazoezi ya Viungo
Huduma za Ustawi wa jamii
Huduma za Upasuaji mdogo na Mkubwa
Huduma za Unasihi
Huduma za Maabara
Huduma za kansa
Huduma za Afya ya Mama na Mtoto
Huduma za mionzi
Duka la Dawa
MIFUMO YA MALIPO YA HUDUMA
Mifumo ya Kielektroni (E-Pay)
Bima Msamaha kulingana na Miongozo
UJENZI WA MAJENGO YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA
Idara Afya ya wilaya ya Meru ina miradi 4 ya ujenzi wa majengo ambayo yametokana na uhaba wa majengo ya kutolea huduma, majengo hayo ni kama ifuatavyo:-
Jengo la huduma ya kinywa na meno
Jengo la wodi ya mama wajawazito
Jengo la huduma ya wajawazito Zahanati ya Kwaugoro
Jengo la Zahanati ya Ambureni.
JENGO LA HUDUMA YA KINYWA NA MENO
Ujenzi wa jengo hili ulianza tarehe 10/03/2017 baada ya makandarasi M/S BIGAN INVESTMENT SONS CO. LTD kushinda zabuni ambayo inajengwa kwa gharama ya Tsh73,594,900 pamoja na kodi hadi kukamilika. Jengo hili lina vyumba viwili vya kutolea huduma ya kung’oa meno na kurekebisha meno, na cha tatu kwa ajili ya upasuaji wa meno na mionzi. Mpaka sasa kiasi cha Tsh. 28,608,864.90 zimelipwa kwa awamu ya kwanza ambapo jengo hili lipo katika hatua ya kupauliwa. Fedha za ujenzi huu zinatokana na mapato ya duka la dawa la nje na mapato ya huduma za Hospitali. Jengo hili likikamilika linaweza kuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa mpaka 30 kwa siku.
Ambapo litanufaisha wakazi wa Meru wapatao 310,480 mara tu jengo litakapokamilika litaanza kazi kwak uwa vifaa vyote muhimu vipo.
JENGO JIPYA LINALOENDELEA KUJENGWA KWA AJILI YA AFYA YA KINYWA NA MENO
JENGO LA MAMA WAJAWAZITO.
Ujenzi huu ulianza tarehe 02/04/2017 Kwa unafadhiliwa na shirika la “World View International “ baada ya andiko (proposal) ilioandikwa na ofisi ya Mganga Mkuu, jengo hili litakuwa na uwezo wa vitanda 30 na chumba cha upasuaji,pamoja na chumba cha watoto njiti. Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi huu ni M/S BIGAN INVESTMENT SONS CO. LTD ambaye atajenga kwa Tsh127,947,500 pamoja na kodi kwa awamu ya kwanza . Hadi sasa ameshalipwa Tsh45,687,950 ambazo zitafikisha ujenzi katika hatua ya lenta pia litakapokamilika litaweza kupokea wajawazito 15 na waliojifungua 15 watoto njiti 10 na kufanya upasuaji kwa wajawazito.
ujenzi huu ni kwa awamu mbili ambapo hatua ya kwanza ipo katika hatua ya kupaua hata hivyo ujenzi huu utakamilika kwa fedha 127,947,500/= kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itategemea nguvu ya mfadhili ili aweze kuendelea nayo. Jengo hili litasaidia wakazi wa Meru wapatao 310,480/=
JENGO LA MAMA WAJAWAWAZITO LINAENDELEA KUKAMILIKA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAMA WAJAWAZITO
MIPANGO YA BAADAYE
Kuendelea kufanya mawasiliano na mfadhili ili aweze kuruhusu fedha za awamu ya pili ya kuongezea jengo hilo
JENGO LA HUDUMA YA WAJAWAZITO ZAHANATI YA KWAUGORO
Jengo hili lilianza kujengwa tarehe 10/04/2016 kwa ufadhili wa “Lions club Tilburg na Wilde Genzen” ulisimamiwa na Adra Tanzania ambapo limegharimu Tsh. 93,00.,000/=likiwa na vyumba 3, chumba cha kusubiria, kujifungulia, pia kina ofisi 2, vyoo 2 vya ndani na bafu 2, jengo hili litaweza kuwekwa vitanda 12 na vya kujifungulia 3 katika jengo hili kunahitajika vitanda 12, kujifungulia 3 na samani kwa ajili ya kutolea huduma.
Jengo kamilika
Mradi huu utasaidia wakazi wapato 2,590 wa kijiji cha kwa Ugoro chenye kaya 558.
Changamoto
Kuna uhitaji wa vitanda vya kusubiria kujifungulia vipatavyo 12
Vitanda vya kujifungulia 3
Na kuna uhaba wa samani katika jengo hilo
Wanufaika
Wakazi 2,590 wa kijiji cha kwa Ugoro ndiyo watakaofaidika na mradi huo, kwani utapunguza safari ndefu kwenda katika huduma ya kujifungua
Mpango wa baadaye
Tunaendelea kuwasiliana na mfadhili ili waweze kutununulia samani na vitanda hivyo
JENGO LA ZAHANATI YA AMBURENI
Kata ya Ambureni ina wakazi 8,799 ambao walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya. Wananchi kwa kushirikiana na WAMATA wamejenga Zahanati ili kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata huduma ya Afya. Jengo hili lilianza tarehe 14/04/2016 ambapo limegharimu jumla ya Sh. 57,000,000/= zikiwepo nguvu za wananchi ambapo wananchi wamechangia kununua kiwanja hicho chenye thamani ya 19,000,000/= (hata hivyo ili Zahanati hii ianze kufanya kazi inahitajika samani vifaa vya kitaalmu na madawa.
JENGO LA UTAWALA
JENGO LA UTAWALA LINALOENDELEA KUJENGWA KWA AJILI YA TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA(CHMT)
MIRADI YA IDARA YA AFAYA
Idara ya Afya ina mradi wa duka la dawa kama chanzo cha kuimarisha huduma na kutatua changamoto ya upungufu wa dawa kwa wagonjwa wanaokosa dawa ndani ya hospitali.
Mradi wa duka la dawa la idara ya Afya unafahamika kwa jina Meru Pharmacy.
CHANGAMOTO
Changamoto za vitendea kazi
Kutokua na chumba cha kuhifadhia miili (mortuary)
Mipango ya Baadaye
Kupelekea vifaa vya tiba vya kuanzia kazi
Kuendelea kuwasiliana na wafadhili na wadau mbali mbali katika kutekeleza majukumu ya idara
WADAU WA IDARA YA AFYA MERU DC
DSW
EGPAF
ENGENDER HEALTH
JHIPIEGO
PATH
STEMM
MARIE STOPES
WORLD VISION
WHO
NHIF
KNCV
PSI
REDCROSS
Ni matumaini yetu kwamba juhudi mbalimbali tunazoendela kuchukua zitasaidia kupunguza uhaba ya miundo mbinu ya kutolea huduma za afya.
AFYA TIBA
Idara inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi,
Majukumu yafuatayo:
AFYA KINGA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Mojukumu hayo ni pamoja na:
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa