Sekta ya kilimo ndiyo inayotegemewa kwa kiasi kikubwa na wakazi wa Halmashauri ya Meru, kwani zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa eneo hili wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Halmashauri ya Meru ina Eneo lenye ukubwa wa jumla ya hekta 126,820, kati ya eneo hilo, linalofaa kwa kilimo ni hekta 81,400 ambapo eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 67,931 sawa na asilimia 84 ya eneo lote la kilimo. Vilevile eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 18,745 na linalomwagiliwa kwa sasa ni hekta 12,810. Mkakati uliopo ni kuendelea kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji kadiri bajeti itakavyoruhusu kwa lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Mazao yanayostawi ni pamoja na; Mahindi, Mpunga, Migomba, Kahawa, Maharage, Maua, Mbogamboga, Matunda, viazi, mihogo, nk.
VYANZO VYA MAJI YA UMWAGILIAJI
Halmashauri ya Meru ina mito 11 na chemchemi 143 ambazo ni vyanzo vya maji ya umwagiliaji na matumizi ya nyumbani. Kupitia baadhi ya vyanzo hivi, Halmashauri imejenga na kuendeleza jumla ya skimu 38 za umwagiliaji ambazo zinatumiwa na wakulima wadogowadogo. Skimu hizi zina hadhi tofauti kiubora. Kila mwaka Halmashauri hutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa skimu hizo kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Kanda za Kilimo
Ukanda huu hupata mvua nyingi za wastani wa milimita 1000 kwa mwaka. Ukanda huu una misitu na vyanzo vya maji yanayotumika katika ukanda wa kati na chini. Mazao yanayostawi ni Kahawa, ndizi, Mahindi, Maharage, Viazi mviringo, Mbogamboga na Matunda.
Ukanda wa kati hupata mvua za wastani wa milimita 500 kwa mwaka. Ukanda huu una misitu ya mtawanyiko na vyanzo vichache vya maji. Mazao yanayostawi katika ukanda wa kati ni Kahawa, Migomba, Mahindi, Mpunga, Maua, Mbaazi, Mihogo, Viazi vitamu, Maharage, Mbogamboga na Matunda.
Hupata mvua za wastani wa milimita 300 kwa mwaka; Kilimo cha umwagiliaji hufanyika kwa kiasi kikubwa katika ukanda huu kwa kutumia maji yanayotoka kanda za juu. Mazao yanayostawi katika ukanda huu ni Mpunga, Mahindi, Maharagwe, Migomba, Mihogo, Mtama, Mbaazi, Viazi vitamu, Matunda na Mbogamboga.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa