IDARA YA MAZINGIRA NA UDHIBITI WA TAKA NGUMU
Idara ya Usafi na Mazingira ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiwa na majukumu makubwa ya Usimamizi wa Mazingira na taka ngumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Kulingana na Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa, Serikali iliidhinisha uundwaji wa Idara ya Usafi na Mazingira kwa ngazi ya Halmashauri, ili kuboresha utendaji mnamo tarehe 1 Julai 2012.
Idara ya Usafi na Mazingira ina vitengo viwili ambavyo ni Hifadhi ya Mazingira na Usimamizi wa taka ngumu. Idara inatekeleza shughuli zake kwa Mujibu wa Sheria za Mazingira namba 20 ya Mwaka 2004 na Kanuni zake, Sheria ya Afya ya Jamii namba 1 ya mwaka 2009 na kanuni zake na sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru za mwaka 2016 (Usafi wa Mazingira na 2014 (Hifadhi ya Mazingira)
Kazi na Majukumu yanayotekelezwa na Idara ya Mazingira na udhibiti taka ngumu ni pamoja na :-
SERA, SHERIA NA KANUNI ZINAZOONGOZA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
Idara ya Usafi na Mazingira inafanya shughuli zake kwa mujibu wa Sera, Sheria Na Kanuni zilizoanzishwa na kupitishwa na serikali ikiwa ni pamoja na; -
Sera ya Mazingira ya Mwaka 1997;
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Namba 20 ya mwaka (2004) na Kanuni zake;
Sheria ya Afya ya Jamii (2009) na Kanuni zake;
Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ya Mwaka 2014;
Sheria Ndogo za Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Meru ya Mwaka 2016.
UZALISHAJI WA TAKA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ina jumla ya wakazi zaidi ya 314,623 kwa mujbu wa sense ya watu na makazi yya mwaka 2012 na maoteo yake. Inakadiriwa kuzalisha jumla ya tani 214 za taka ngumu kwa siku. Kiwango hicho cha uzalishaji kinajumuisha taka za majumbani, viwandani, taasisi, sehemu za biashara, masoko na taka kutoka sekta isiyo rasmi.
UWEZO WA KUKUSANYA NA USAFIRISHAJI TAKA KUPELEKA DAMPO
Halmashauri ya wilaya ya Meru kupitia kwa mawakala walioteuliwa kwa kufuata utaratibu wa muongozo wa sheria ya Manunuzi ya mwaka 2013, ndiyo hutoa huduma ya kukusanya na kuondoa taka katika maeneo ya makazi, Masoko, biashara, maeneo ya wazi na katika Taasisi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kutumia magari yao kwenda katika dampo/shimo la taka.
MIKAKATI YA IDARA KATIKA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupitia Idara ya Mazingira na Usimamizi wa taka ngumu imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuboresha utunzaji wa mazingira.
Mikakati hiyo ni pamoja na; -
Kuhakikisha kwamba elimu juu ya Hifadhi ya mazingira kwa wadau mbalimbali inafanyika ili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira katika Halmashauri.
Kwa kushirikiana na Idara zingine Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana na utunzaji na usimamizi wa mazingira zinatekelezwa tokea ngazi ya kaya hadi wilaya na taifa kwa ujumla.
Kufuatilia na kuainisha na kusimamia sheria kwa ajili ya maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa kama maeneo yenye chepechepe za maji (Ardhi oevu), kandokando mwa kingo za mito, milima ya hifadhi ya jamii, na maeneo mengine yenye thamani mbalimbali ya uhifadhi.
Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu usimamizi na utunzaji wa Mazingira.
Kushiriki katika usimamizi wa miradi mbalimbali inayofanyika katika Halmashauri katika kuhifadhi Mazingira kabla ya mradi kuanza na ukaguzi wa mara kwa mara wakati Mradi ukitekelezwa (regular project mornitoring) kwa kufuata sheria mama ya hifadhi ya mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 ili kuhakikisha mazingira hayaharibiwi; mfano miradi ya ujenzi wa miundombinu, Mashule, Minara, uchimbaji wa Mchanga, mahoteli, mashamba makubwa ya maua na mbogamboga na mengineyo.
Kuunda kamati za kuhifadhi mazingira kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Wilaya.
Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa viongozi, watendaji na kamati za Mazingira.
Halmashauri mwaka 2018 ilianzisha kampeni endelevunashirikishi ya uhifadhi na usafi wa mazingira ambayo inaomba kila madau kushiriki kwa namna ambaye anaona kwake inafaa. Kampeni hii ina kauli Mbiu inayosomeka Safisha na Pendezesha Meru yetu “KEEP MERU CLEAN AND GREEN”
3.1.2 Kuboresha utunzaji wa taka sehemu zinapozalishwa
Moja ya tatizo la kuzagaa taka ovyo ni ukosefu wa vifaa vya kuhifadhia taka katika sehemu zinapozalishwa. Kuwepo kwa vifaa hivyo kama mapipa ya taka, mifuko ya plastiki au kontena kutasaidia kuweka mazingira ya makazi na biashara katika hali ya usafi na kupunguza gharama za uzoaji taka. Jamii itahamasishwa kutunza taka katika ngazi ya kaya na kuacha tabia ya kutupa taka hovyo kila zinapozalishwa pale inaposhindikana hatua za kisheria zitakuwa zinachukuliwa.
Kuwa na mfumo imara na endelevu wa usimamizi wa Sheria
Kila Mtaa, Kijiji na Kata utakuwa na mfumo wa ushirikishaji wa wakazi katika usimamizi wa sheria za usafi wa mazingira ni muhimu. Hivyo ili kupata ushirikiano huo ni kutakuwepo na wasimamizi maalumu wa sheria za usafi katika ngazi ya Mtaa,Kijiji na Kata na kamati za Afya na Mazingira ambao watahakikisha kila mkazi na mfanyabiashara anazingatia kanuni na sheria za afya kama vile kudhibiti utupaji taka na maji taka hovyo, kuhimiza wakazi kusafisha maeneo yanayozunguka nyumba na mfereji unaopita mbele ya nyumba n.k...
Wasimamizi hawa wa kijamii watafanya kazi zao chini ya Afisa Mtendaji wa Mtaa/Kata na mashauri yote ya uendeshaji wa kesi yatafanyika katika baraza la Kata. Afisa Afya wa Kata ndiye atakuwa mtaalamu katika kutoa miongozo ya kazi siku hadi siku katika ngazi ya Kata.
3.1.3. Ushiriki wa Sekta nyingine kusaidia kuboresha mandhari ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Pamoja na kwamba Halmashauri ina sheria ndogo na
linaweza kutunga sheria nyingine; bado mfumo wa ukaguzi na usimamiaji wa sheria hizo bado ni hafifu; lakini pia ili kupendezesha Halmashauri, sekta ya Mazingira na Usafishaji haistahili kusimama peke yake kwani bado kuna sekta kama Maendeleo ya Jamii inayopaswa kutekeleza mkakati wa kuhamasisha ushiriki wa jamii, sekta ya uhandisi inayopaswa kuangalia suala zima la miundombinu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa njia za waendao kwa miguu (pavements) pembeni ya barabara kupunguza michanga, sekta ya maliasili inatakiwa kupanda miti na maua na kuikatia (prunning) ili kupendezesha mandhari ya Halmashauri n.k.
Kutoa elimu na mipango ya ushirikishwaji wakazi
Kutoa elimu kwa wakazi ni muhimu ili kupata ushirikiano wao. Hivyo mipango ya jinsi ya kuelimisha jamii na kutoa taratibu mbalimbali za usafishaji na uzoaji taka kama majukumu na wajibu wa kila Mdau, siku za uzoaji na sehemu za kuweka taka, matumizi ya vifaa mbalimbali vya kutunzia taka, utunzaji wa mandhari ya halmashauri n.k. kutasaida katika kutekeleza kazi za usafishaji kwa ufanisi zaidi na kuwa endelevu. Katika kutekeleza mkakati huu kutakuwa na vipindi vya uhamasishaji jamii kupitia vyombo vya habari hasa radio FM zilizopo katika Jiji la Arusha, mikutano ya hadhara ya Mitaa, Vijiji na katika maeneo yenye mikusanyiko yenye watu wengi
Kuboresha Ukusanyaji wa ada ya taka kila mwezi
Mfumo wa utoaji wa huduma za usafishaji na kuzoa taka utafanikiwa tu; kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba wakazi na wafanyabiashara wanachangia huduma ya uzoaji taka wanayoipata. Kwa mujibu wa sheria ndogo ya usafishaji na ulipaji ada, Halmashauri limeweka utaratibu na viwango vya ada ya taka; katika utaratibu huu, kila kaya na majengo ya biashara, kampuni na taasisi inatakiwa kulipa ada ya taka kila mwezi kupitia kwa mawakala wa usafishaji mazingira.
Kuboresha eneo la kutupia taka
Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetenga eneo la Hekta 100 katika kijiji cha Valeska kwa ajili ujenzi wa Miundombinu ya kudumu ya kisasa ya kutupia taka yaani “LANDFIL”. Kwa kuwa inahitaji gharama kubwa za ujenzi na Halmashauri yenyewe haitaweza tunawakaribisha wadau wote wenye nia njema kusaidia Halmashauri katika ujenzi ya Miundombinu hii.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa