Msitu wa Usa springs ambao pia hujulikana kwa jina la kiasili kama Kibola upo Kaskazini mwa mji wa Usa River takiribani umbali wa kilomita tatu kutoka Mji wa Usa River.
Msitu huu unamilikiwa na Halmashauri ya Meru na una ukubwa wa ekari 21 na umezungukwa na vijiji vitatu vya Nkoanekoli, Sangananu na Kiwawa.
Vivutio vya Watalii vilivyopo kwenye Msitu wa Usa Springs
Msitu wa Usa springs umezungukwa na hotel nyingi za Kitalii kama vile Ngurdoto Mountain Lodge, Ngurdoto View, Shangazi Hotel, Mbega Lodge, Kiboko Lodge, River Tree na Arumeru River Lodge.
Shughuli za kitalii huwa zinafanyika katika msitu huu na Watalii wamekuwa wakitembezwa katika msitu huo.
Uwekezaji unaotakiwa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa