Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa kilomita 126.3 katika Wilaya ya Arumeru ambapo umezindua, kukagua , kuweka jiwe la msingi, na kufungua miradi tisa katika sekta ya TEHAMA, elimu ,afya, maji, barabara, kilimo na uwekezaji yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3.
Aidha, Wilaya ya Arumeru ilipokea Mbio Maalum za Mwenge siku Jumamosi tarehe 19 Juni 2021 toka Wilaya ya Arusha na kukimbiza Mwenge wa Uhuru umbali wa Kilomita 126.3 katika Halmashauri mbili za Arusha na Meru na leo tarehe 20 Juni, 2021 Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa kwa Wilaya ya Longido.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luten Josephine Paul Mwambashi amepongeza vijana wa Kikundi Cha Umoja Youth Group kwa kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri kujipatia maendeleo kwa kukuza mtaji kutoka Milioni 6 hadi shilingi milioni 48.
Luten Josephine ametoa wito kwa vijana kuendelea kufanya Kazi kwa bidii na kujipatia kipato halali na kushiriki kikamilifu kujenga uchumi wa taifa.
Aidha, Mwenge wa Uhuru umetembelea Mradi Wa TEHAMA unaotumika kujifunza na kufundishia, umekagua na kuzindia mradi wa ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa katika shule ya Sekondari Kikwe, umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara kiwango Cha lami Sangisi-Nambala, umetembelea Kituo cha kuuzia mafuta kwa rejareja , umetembelea Mradi wa kilimo cha migomba na tumbaku na umezindua jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Oltrument. Aidha, umekagua mradi wa ujenzi wa bwalo shule ya Msingi Ilboru na kutembelea mradi wa Kikundi Cha Vijana cha "Umoja youth group".
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 ni “TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu; itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa