Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Meru lajikita katika mikakati ya kuongeza mapato mapato ya Halmashauri hiyo kwa kudhibiti vyanzo vya mapato sambamba na kubuni vyanzo vipya.
Wakichangia wakati wa kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo lilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano ,Madiwani wamesema kunahaja ya kuboresha ukusanyaji katika vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na kuwalete wananchi maendeleo’’Tunahaja ya kujiridhisha na makusanyo ya mapato katika mnada wa kikatiti ili kupata uhalisia na ikiwezekana boresha mnada huo kuongeza mapato’’ameeleza Mhe. Kisali Nyiti, diwani wa Kata ya Kikatiti .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Jeremia Kishili ametoa wito kwa Madiwani kushirikiana na wataalumu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato katika Kata zao sambamba na kudhibiti mianya ya baadhi ya wafanya biashara wanaokwepa tozo na shuru mbalimbali .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya yaMeru Ndg. Emmanuel Mkongo amesema kwa mwaka wa fedha 2020 /2021 Halmashauri hiyo ilipitisha kukusanya Shilingi Bilioni 3.4 ambapo mpaka mwezi Desemba Halmashauri hiyo ilikusanya asilimia 50% ,pia amesema kumekua na changamoto katika ukusnyaji kwa vyanzo vilivyopo akitoa mfano wa chanzo cha ushuru wa huduma ambapo wanategemea hoteli za kitali ulishuka kutokana na janga la Virusi vya CORONA.
Mkongo amesema watashirikiana na madiwani kuhakikisha wanakusanya mapato kwa asilima moja na kuwaletea wanachi maendeleo.Pia amejibu swali lililohojiwa na baadhi ya madiwani juu ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa kueleza kuwa Halmashauri hiyo kupitia fedha za mapato yake ya ndani (Own Source) imetumia zaidi ya Shilingi Milioni 160 kununua vifaa vya ujenzi ambavyo ni Bati 1860 zilizogharimu shilingi 48,259,004.51, Mbao shilingi 64,598,752.00 na Saruji mifuko 3325 iliyogharimu shilingi 48,212,500.
Baadhi ya picha za tukio.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremiah kishili akizungumza wakati wa mkutano.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya yaMeru Ndg. Emmanuel Mkongo akizungumza wakati wa mkutano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa