Taasisi ya kifedha ya Faidika kwa lengo la kutumia faida yake katika suala zima la kurahisisha utoaji huduma kwa watumishi wa Umma imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni tatu na laki saba ambavyo ni Printa yenye uwezo wa kudurufu,kuskani na kuprinti nyaraka pamoja na komputa .
Akizungumza na wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya fedha Faidika Ndg.Baraka Munisi ,amesema kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma kupata huduma ya Mkopo kupita Faidika kwani Mahesabu ya kiwango cha kulipa yanafanyika kupitia mfumo wa kitaalam na hakuna makosa ya kibinadamu hivyo mteja atalipa kiasisi anachodaiwa tu ,pia taasisi ya Faidika hutoa mkopo kwa mteja wake ndani ya masaa 24, na makato ya mikopo ya faidika huzingatia viwango vilivyo izinishwa na Serikali hivyo mteja ana bakiwa na kiwango cha mshahara baada ya makato yote kwa mujibu wa sheria.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi Grace Mbilinyi ameishukuru taasisi ya fedha ya Faidika kwa kuchangia maendeleo ya Halmashauri hiyo kwa kuongeza vitendea kazi vitakavyo leta tija kwenye kuwahudumia watumishi haswa kwenye uingizazi wa makato ya watumishi kwenye taasisi za fedha kupitia mfumo wa (HCMIS).
Makao makuu ya Taasisi ya fedha ya Faidika ijulikanayo kama Letshego Group yapo Dar ES Salaam jengo la Vodacom Tower Gorofa na 3.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya fedha Faidika Ndg.Baraka Munisi kizungumza na wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya fedha Faidika Ndg.Baraka Munisi akikabidhi vifaa kwa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru,ambaye ni Mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Bi.Grace Mbilinyi.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi wa Faidika na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru pamoja na watumishi toka taasisi hizo.
Baadhi ya Watumishi wakati wa makabidhiano ya vifaa.
Wakuu wa Idara,Vitengo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa makabidhiano ya vifaa .Kulia ni mtumishi wa taasisi ya fedha ya Faidika.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi wa Faidika na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru,wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Meru pamoja na watumishi toka taasisiya Faidika.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa