Neema kwa Jimbo la Arumeru
Dkt.John D. Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wakati akikabidhiwa mabomba ya mradi wa ukarabati wa maji amesema Serikali imezidi kushusha neema katika Jimbo hilo kwa kutoa shilingi milioni 438 kwaajili ya ukarabati miundombinu chakavu ya maji katika Kata za Kikatiti, Kikwe, Maji ya Chai na Ngarenanyuki.
Dkt. Pallangyo , amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya maji na miundombinu ya barabara Jimboni humo kwa kutoa tena shilingi bilioni 2 kwaajili ya miradi ya maji sambamba na kutoa shilingi bilioni Moja kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Malula -Ngarenanyuki.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Eng.Richard Ruyango amempongeza Mheshimiwa Mbunge Pallangyo kwa ufuatiliaji wa maendeleo ya watu wa Meru ambapo amemwagiza Meneja wa Wakala wa Maji Vijiji na Mjini (RUWASA) kuhakikisha Wananchi wanapewa elimu ili wawe na uelewa wakati wa utekelezaji na ukarabati wa miradi hiyo .
Eng.Ruyango amewataka Wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji na kutunza miundombinu ya maji kwani Wilaya hiyo itawachukulia hatua wote watakao jaribu kwa namna yoyote kuhujumu miradi ya maji kwa kuharibu miundombinu.
Mheshimiwa Aminiel, Diwani wa Kata ya Ngarenanyuki ameishukuru Serikali kwa maboresho ya miradi hiyo mikongwe ya ya maji pamoja na kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya miradi mingine ya maji katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
Kadhalika,Aminieli ametoa wito kwa wanachi kupokea miradi hiyo yenye manufaa makubwa na kuwa wao kama Viongozi watasimamia na kuitunza miradi hiyo.
Eng. Shabir Waziri, Meneja wa RUWASA amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumpata mkandarasi na Wanachi walishapewa elimu kipindi cha usanifu wa miradi na elimu hiyo itaendelea kutolewa
Mbunge Dkt.John D. Pallangyo akiwasili makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Makabidhiano ya mabomba kwaajili ya miradi ya maji.
Dkt.John D.Pallangyo akizungumza na Eng.Shabiri Waziri Meneja wa RUWASA Arumeru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa