Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kichama Meru imeridhia taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kipindi cha Julai hadi Desemba 2020.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kichama Meru Mhe.Furaini Mungure amepongeza utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo katika uwezeshaji wa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kiuchumi kwa kipindi cha Julai hadi Disemba imetoa mkopo wa Shilingi Milioni 134 kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Aidha, Mhe.Mungure amewataka viongozi wa Serikali kuwashirikisha Viongozi wa ngazi za chini katika masuala mbalimbali ikiwemo utatuzi wa migogoro.
Eng.Richard Ruyango, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amewataka Viongozi kuhakikisha wanatatua migogoro na kero katika maeneo yao ili wananchi wasipoteze muda na gharama za nauli kutafuta suluhu ambazo wangeweza kupata kupitia Viongozi wa maeneo yao.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt. John D.Pallangyo amemshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusikia kilio cha wanachi wa Jimbo hilo ambapo mbali nakuongeza milioni 500 kwenye bajeti ya kukarabati miundombinu ya barabara ametoa shilingi Bilioni Moja kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Malula-Ngarenanyuki.
Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ametoa wito kwa wajumbe wa Mkutano huo kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za kiuchumi na kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri na kujiletea maendeleo.
Mkutano huo Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kichama ya Meru umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhudhuriwa na Wajumbe wapatao 148 kutoka katika Kata 27 za kichama.
Kupitia Mkutano huo Watalaam wa Sekta mbalimbali ikiwemo Wakala Barabara Vijijini na Mjini ( TARURA), Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Wakala ya Maji Vijijini na Mjini (RUWASA) na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha wanaosimamia mradi wa maji wa zaidi ya Bilioni 500 ambao miundombinu yake inajengwa katika Halmashauri ya Meru waliwasilisha taarifa za Sekta zao na kutoa ufafanuzi wa Hoja za Wajumbe.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kichama Meru akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kichama Meru Mhe.Furaini Mungure akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru.
Eng.Richard Ruyango Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru.
Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili akihimiza ushirikiano zaidi Kati ya Madiwani na Watendaji katika kutatua kero za wananchi.
Ndg.Emmanuel Mkongo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Meru
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Meru
Wajumbe waalikwa wa Mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Meru
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Meru
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Meru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa