Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amevieleza vyombo vya habari kuwa,kufuatia upepo mkali uliotokea jana majira ya mchana Mkoani Arusha ambao ulienea mpaka katika maeneo ya Wilaya ya Arumeru umesababisha madhara ambapo Katika Halmashauri ya Meru ,watu watatu waliokolewa baada ya mitumbwi miwili waliokuwa wanautumia katika Ziwa Momela kupigwa na upepo na kupinduka, ambapo kijana mmoja alietambuliwa kwa jina la Samwel Gildati Mhina anaejishughulisha na kazi za kuongoza watalii anahofiwa kuzama katika ziwa hilo pamoja na mtumbwi aliokuwa anautumia haujapatikana mpaka sasa, vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka mkoani na wilaya ya Arumeru vinaendelea na kazi ya kumtafuta.
Katika tukio hilo raia wawili ambao wametambuliwa kwa majina ya Dkt.Tuemper Bern John na Dkt.Rosenberger Raia wa Ujerumani waliokolewa mara baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba ya upepo na kupinduka pamoja
Aidha Muro amesema zoezi la uokoaji linaendelea,pia kuna madhara mengine ya upepo huo katika Halmashauri ya Meru yametokea katika Kijiji cha Kimundo Kata ya Nkoarisambu ambapo Nyumba moja imeezuliwa paa pia katika kijiji cha Ulong’aa kata ya Nkwandrua paa la choo cha shule ya msingi nalo liliezuliwa.
*waliookolewa ni wazima, wanaendelea na shughuli zao
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Mkuu wa W
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa