Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa wito kwa Wenyeviti wa Vijiji Halmashauri ya Meru kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Serikali "ushirikiano katika kazi ndio hufanya kazi kukamilika kwa wakati na kuleta tija kwa Wananchi"amehimiza Mhe.Ruyango
Ruyango ametoa wito huo wakati wa kikao cha kuendelea kufahamiana ikiwa ni pamoja na kukumbushana wajibu na Majukumu .
Wakichangia kwa nyakati tofauti Wenyeviti hao wa Vijiji wamempongeza Mkuu wa Wilaya na Uongozi wa Halmashauri hiyo kutoa nafasi hiyo ya kukutana "Tumefurahi kupata kikao hiki tunaomba tupewe Mafunzo na kujengewa uelewa wa kina wa usimamizi na utekelezaji wa shughuli za Serikali "amesema Chirtopher Pallangyo Mwenyekiti wa kijiji cha Migandini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Vijiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mwl.Zainabu Makwinya ametoa wito kwa Wenyeviti wa Vijiji kutoa ushirikiano kwenye ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambayo hutumika kuleta maendeleo kwenye Maeneo yao "Wenyeviti wa Vijiji wananafasi kubwa kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanyika"amehimiza Makwinya
Naye Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amesema atawasilisha baadhi ya Wenyeviti wa Vijiji ALAT .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na wenyeviti wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Mwenyekiti wa kijiji cha Migandini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Vijiji Chirtopher Pallangyo akizungumza wakati wa Kikao .
Wenyeviti wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .
Wenyeviti wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa