• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

DC ARUMERU AWATAKA WALIOVAMIA MILIMA KUONDOKA MARA MOJA

Imewekwa: May 10th, 2023

Mkuu wa Wilaya  ya  Arumeru  Mhe. Emmanuela  Kaganda  ametoa  wito  kwa wananchi  kutunza vyanzo vya maji na mazingira ambapo pia  amewataka wanaofanya shughuli za kibinadamu  katika milima kuacha mara moja kwani Serikali wilayani humo haitowafumbia macho.

Mhe.Kaganda amesema hayo wakati akiwaongoza wananchi  wa Kata ya Mbuguni Halmashauri  ya  Meru,  kupanda miti kwenye kingo za korongo la mto Nduruma ambalo Serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan  ilitoa zaidi ya Milioni 200 za kufukua korongo hilo na kutatua changamoto ya mafuriko iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kata hiyo ya  Mbuguni na Shambarai Burka.


Mhe.Kaganda amesema Wilaya ya Arumeru imebarikiwa kuwa na vyanzo Vingi vya maji vinavyoanzia milimani, hivyo wananchi hawana budi kuvitunza kwa manufaa yao na manufaa ya wengine " Wazee wetu walitunza vyanzo hivi nasi tunapaswa kuvitunza kwa ajili ya kizazi kijacho"amehimiza Mhe Kaganda


Naye, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya  Wilaya  ya  Meru  Mwl  Zainabu Makwinya  amesema Halmashauri  hiyo inahakikisha inaunga mkono juhudi za Serikali katika agenda ya utunzaji mazingira na vyanzo vya maji, ambapo awali  kupitia mapato yake ya ndani Waheshimiwa madiwani waliridhia kutoa Milioni 26 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwenda kuchimbua Korongo hilo la mto Nduruma.

Nao Waheshimiwa  Madiwani wa Kata za Shambarai na Mbuguni ambazo awali zilikuwa zikisumbuliwa na mafuriko wameishukuru Serikali kufukua Korongo hilo na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji.

Tito Kitomari kutoka Bonde la Pangani ametoa Wito kwa jamii kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwani hakuna mbadala wake ambapo amebainisha Bonde la Pangani kuendelea kushirikiana na Jamii na Serikali  katika utunzaji wa vyanzo vya maji.





Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI September 17, 2023
  • Aprili 2023 Mwisho wa Kukamilisha Malipo viwanja/ Mashamba mradi wa Valeska April 18, 2023
  • WIKI YA CHANJO KIANZA TAREHE 24 HADI 30 APRILI 2023 April 24, 2023
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI MERU ATEMBELEA SOKO JIPYA LA MAJI YA CHAI

    September 18, 2023
  • SATACOFO YATOA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA HALMASHAURI YA MERU

    September 15, 2023
  • DR. BITEKO AFUNGUA KONGAMANO LA TAASISI ZA ARDHI AFRIKA- ARUSHA

    September 12, 2023
  • KIKOSI 833 WATAKA MAFUNZO YAONGEZWE MUDA KWA MIEZI 6

    September 11, 2023
  • Tazama Vyote

Video

MKURUGENZI MAKWINYA AFUNGUA MAFUNZO YA KUIMARISHA TIMU ZA AFYA MOJA
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa