Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Ndg. Jerry Muro ametimiza ahadi ya kuijengea nyumba familia ya Eliud Samwel Nyari ambayo ilikumbwa na janga la nyumba yao ya mbao kuteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtoto wao mdogo Mercy Eliud Nyari
Dc Muro ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba hiyo ambayo imejengwa katika kiwanja kingine jirani na makazi yao ya zamani yaliyoteketea ambapo safari hii wamejengewa nyumba ya matofali ya vyumba vitatu ambayo imekamilika kwa kiasi kikubwa na kuanza kutumiwa kama makazi mapya ya familia hiyo uku kukiwa na sehemu za nje za mifugo na sehemu ya kupikia chakula.
Mama wa familia hiyo Bi Rogathe Nyari amesema yeye alikuwa akisikia tu kazi nzuri za ujenzi jamii bora ya wananchi wa Arumeru zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro na sasa ameamini kwa macho kile alichokuwa akikisikia kuhusu Ndugu Muro
Mama wa familia hiyo Bi Rogathe Nyari amesema yeye alikuwa akisikia tu kazi nzuri za ujenzi jamii bora ya wananchi wa Arumeru zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro na sasa ameamini kwa macho kile alichokuwa akikisikia kuhusu Mkuu wa Wilaya Jerry Muro
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alipotembelea na kutoa pole kwa Familia ya Eliud Samwel Nyari ambayo ilimpoteza mtoto kutokana na nyumba yao kuteketea kwa moto .
Nyumba Mpya aliyojengewa familia ya Bi Rogathe Nyari
Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro alipoitembelea familia ya Bi Rogathe Nyari
Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro alipoitembelea familia ya Bi Rogathe Nyari
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa