DED MERU AWASILISHA TAARIFA KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI.
Imewekwa: March 13th, 2024
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo na kueleza kuwa, Serikali imeweza kutoa shilingi 7,801,765,956.90 kwa ajili ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na miradi katika Sekta mbalimbali zinazotoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo Shule za Msingi, Sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za Afya .
Aidha, amesema kuwa, Halmashauri imeweza kuchangia shilingi 760,198,360.01 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata na Vijiji hadi kufikia mwezi Februari 2024 ambayo ni sawa na asilimia 40.7 ya makusanyo halisi.
Kuhusu mradi unaokaguliwa na Kamati ya kudumu ya Bunge TAMISEMI, mradi wa ujenzi na ukarabati wa majengo katika Hospitali ya Wilaya ya Meru, Mwl. Zainabu amesema kuwa, Mradi huo umepokea shilingi Milioni 900,000,000.00 kwenye akaunti ya Hospitali na ujenzi umeanza kwa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, kichomea taka cha kisasa, jengo la Famasia pamoja na ukarabati wa wodi ya watoto.
Mwl. Zainabu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha hizi kwani zitaongeza ufanisi katika utoaji Wa huduma za afya kwa ustawi wa wananchi wa Meru.