Wananchi wa Kata ya Mbuguni Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha huduma za Afya ikiwemo upatikanaji wa dawa.
Wananchi hao wamemweleza hayo Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mhe.Mrisho Gambo alipotembelea kituo cha Afya mbuguni wakati wa ziara yake ya siku Moja katika Halmashauri hiyo.
Wananchi hao wamesema hapo awali huduma katika kituo hicho zilikua za kusuasua na kunawakati walikosa dawa jambo lililokuwa kero kubwa,"Tunaishukuru serikali kwani sasa tunahudumiwa vizuri na hatujawahi kukosa dawa katika kituo hiki" kauli ya Perpetua Maphie mkazi wa mbiguni.
Sambamba na pongezi hizo wananchi hao wamemwomba Mhe.Gambo kuwasaidia kupata gari la kubebea wagonjwa na kutatua kero ya uhaba wa watumishi.
Aidha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara ameeleza kuwa upatikanaji wa dawa katika Halmashauri hiyo ni zaidi ya asilimia 90% .
Dkt.Kilasara amesema upatikanaji huo wa dawa unaoridhisha ni baada ya Serikali ya awamu ya Tano kuiongezea Halmashauri hiyo bajeti ya dawa toka milioni 49 hadi milion 422 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni milioni 553.
Mhe.Gambo ameridhishwa na ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Usa-River pamoja na hali ya upatakanaji wa dawa kwa Mkoa wa Arusha ikiwa ni ongezeko la bajeti ya dawa toka milioni 2061 hadi bilioni 2 na milioni 400.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Meru Dkt.Cosmas Kilasara akitoa maelezo juu ya chumba cha maabara katika kituo cha afya Mbuguni wakati wa ziara ya Mhe.Gambo.
Mwonekano wa chumba cha upusuaji katika kituo cha Afya Mbuguni.
Mkusanyiko wananchi wa Mbuguni wakati wa ziara ya Mhe.Gambo katika kituo cha afya mbuguni
Perpetua Maphie Mkazi wa Mbuguni.
Wodi ya mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Usa-River.
Jengo la upasuaji katika kituo cha Afya Usa - River.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa