Jamii yaaswa kuhakikisha wajawazito wanawahi kufika katika vituo vya huduma za afya ili kuepusha vifo na madhara kwa watoto wachanga.
Akizungumza wakati wa kikao cha kujadili vifo vitokanavyo na Uzazi na kujifungua katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Jackline Urio ambaye ni Daktari bingwa wa Magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Mt.Meru amesema kuna uwezekano mkubwa mtoto kuzaliwa akiwa na uharibifu wa selihai za ubongo na kupelekea ulemavu wa kudumu pia kupoteza maisha endapo mama mjamzito atachelewa kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa wakati.
Dr. Urio ametoa wito kwa jamii kuachana na dhana potofu ya mama mjamzito kusubiri hadi hatua ya kujifungua ndipo aelekee hospitali kwani ni miongoni mwa sababu za vifo vya mama wajawazito na watoto "kinamama acheni dhana ya kusubiri uchungu wa kujifungua ndipo uelekee kituo cha kutolea huduma za afya" amehimiza Dkt.Urio
Aidha Dkt.Urio amefafanua kuwa kuwahi katika vituo vya huduma kuna imarisha afya ya mama na pia uwezekano mkubwa wa wataalamu wa afya kuweza kuokoa maisha ya watoto wachanga pamoja na mama .
Mwakilishi wa Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Bi. Vones Uiso amesema Serikali katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi imeanzisha mpango wa kuhakikisha viongozi wa ngazi ya jamii wanashirikishwa kwa karibu katika swala zima la kujadili huduma za afya.
viongozi ngazi kijamii wamepongeza ushirikishwaji wao na kutoa wito kwa baadhi ya wananchi ambao ni wakunga wajadi wasio na mafunzo ambao hawajatambuliwa kwa taratibu za afya wanaochangia kinamama wajawazito kujifungulia majumbani kuacha kwani serikali itawachukulia hatua kwa kuhatarisha maisha ya kinamama .
Ndugu Ten ambaye ni Afisa Tarafa ,Tarafa ya Mbuguni amesema kuna umuhimu mkubwa wa elimu ya afya ya uzazi hivyo wataalamu wa afya afya ngazi ya Kata kushirikiana na Wilaya hawana budi kutoa elimu ya kina kuhusiana na afya ya uzazi.
Naye Mratibu wa afya ya Uzazi katika Halmashauri ya Meru Bi. Sikudhani Mkama amesema pamoja na kupungua kwa vifo vya kina mama kutoka 6 mwaka 2019 hadi 1 mwaka 2020 bado idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 imeongezeka kutoka 34 mwaka 2019 hadi 41 mwaka 2020.
Pia. Mratibu huyo amesema kunauwezekano mkubwa wa idadi hiyo kuongezeka kwani mwenendo wa viashiria vya hali ya afya ya uzazi hususani Kiashiria cha idadi ya wanaojifungulia vituoni ni asilimia 58% ambapo ni chini ya lengo la kitaifa,"tuwahimize kinamama wajifungulie vituo vya huduma kuepuka vifo vya watoto wachanga"amesisitiza Sikudhani.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dr Maneno Focus amewataka waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma kuzingatia maagizo yanayotolewa na viongozi mbalimbali ikiwemo kusimamia huduma kwa weledi na maadili ili kuleta tija kwenye utoaji wa huduma za afya, Pia.kusimamia mapato na kuinua viashiria muhimu vya huduma kwa zaidi ya asilimia 20 katika robo ya mwaka januari hadi machi 2021.
Aidha Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru kikiwajumuisha kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT).Maafisa Tarafa,wadau wa afya na watendaji wa kata, kilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro ambaye aliwataka maafisa tarafa, Watendaji waVijiji na Kata sambamba na Viongozi wa Idara ya afya kuhakikisha wanahimiza wananchi kujiunga na Mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboresha ICHF ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma bora za afya.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya watoto Jackline Urio.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Maneno Focus
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Mratibu wa afya ya Uzazi katika Halmashauri ya Meru Bi. Sikudhani Mkama
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Afisa Tarafa Mbuguni Bw. Abdalah Teni akizungumza wakati wa kikao .
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa