Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo ametoa Wito kwa wananchi wa Halmashauri hiyo kuzingatia elimu na ushauri toka kwa wataalam wa afya ili kuwa na afya bora wakati wote.
Mkongo amesema hayo katika maadhimi sho ya wiki ya kudhibiti na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa Halmashauri hiyo yamefanyika katika Kata ya Mbuguni na kitaifa yamefanyikia Mkoani Dodoma.
Mkongo Amesema kwa miaka ya hivi karibuni vifo vingi vimetokana na magonjwa yasiyo ambukizwa hali inayopelekea Serikali kuanza kampeni hiyo ya kuyathibiti.
Katika kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu kwa wakati Mkongo amewaagiza waganga wafawidhi wa vituo vya afya katika Halmashauri hiyo kutenga siku moja katika Juma ya kliniki ya magonjwa ya Sukari na shinikizo la juu la damu kwani ni taarifa zinaonesha zaidi ya wagonjwa 5000 waligundulika kuwa na maradhi hayo kwa mwaka 2018.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Maneno Focus amesema miongoni mwa visababishi vya magonjwa yasiyoambukizwa ni pamoja na lishe isiyofaa, kutofanya mazoezi,unywaji wa pombe kupita kiasi,uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku,na sababu nyinginezo za kurithi.
Drk.Focus alifafanua kuwa Mpango wa Kuzuia magonjwa yasioambukizwa umelenga kuelimisha na kuihusisha jamii,kuwapa mafunzo watoa huduma na kuongeza vifaa tiba na dawa katika ngazi zote za kutolea huduma.Katika Zoezi la wiki ya udhibiti wa Magonjwa yasiyoambukiza halmashauri ya Meru iliwaalika madaktari bingwa wa magonjwa ya Ndani na upasuaji ambao walitoa ushauri na tiba kwa wananchi zaidi ya 798 kutoka kata za pembezoni zikiwemo Leguruki,Ngarenanyuki na Mbuguni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru akizungumza na wananchi wa Mbuguni ,Kulia kwake ni Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mbuguni Ndg.Abdallah Temi na kushoto ni Mganga Mkuu Wilaya Dkt.Focus Maneno.
Wananchi wa Kata ya Mbuguni wakati wa uzinduzi wa wiki ya kudhibiti na kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa.
zoezi la upimaji Kata ya Leguruki
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa