• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KAMATI YA SIASA YAWATAKA WAHANDISI KUWATUMIA MAFUNDI WENYE UJUZI

Imewekwa: June 30th, 2021

Kamati ya Siasa Wilaya ya Kichama ya Meru imewataka Wahandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  kuwatumia mafundi wenye ujuzi na wazalendo katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali sambamba na kufuatilia kwa karibu ujenzi na kuhakikisha mafundi wamefanya kazi kwa mujibu wa BOQ na maelekezo ya kitaalam kabla ya kulipa fedha kwa kila awamu na fedha za zuio.


Kamati ya Siasa imeelekeza Wahandisi kufuatilia na kuwasimamia mafundi kwa ukaribu ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vilivyowekwa. Maelekezo hayo yametolewa kutokana na changamoto ndogo ndogo zilizobainika katika ukaguzi wa baadhi ya Miradi .


Hayo yamejiri wakati Kamati ya Siasa ilipotembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu(3) katika Shule ya Msingi  Kerikenyi ambao umefadhiliwa na Serikali Kuu kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).


Aidha, Kamati imewashukuru wafadhili wa miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kutoa Wito kwa wafadhili hao kuwatumia Wananchi  katika utekelezaji wa miradi ili miradi hiyo kuwa na tija zaidi kwa kutekelezwa kwa gharama nafuu na kuongeza wigo wa kutekeleza miradi mingi zaidi.


Kamati imepongeza ujenzi wa Vyumba manne (4) vya  Madarasa katika Shule za Sekondari Mbuguni na Majengo na ambayo yameonekana kusimamia vyema na wahandisi wa ujenzi ambapo  Kamati imepongeza uongozi wa Vijiji, Kata na Halmashauri kwa ushirikiano na usimamizi mzuri wa miradi.


Pia. Kamati ya Siasa imempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo kwa msimamo imara wa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Serikali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya katika Halmashauri hiyo .


Ikiwa ni siku ya 3 na ya Mwisho ya ziara ya Kamati ya siasa baada ya kutembelea na kukagua miradi 18 katika sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Ufugaji, Uchumi na Uzalishaji mali, Kamati imeelekeza  Halmashauri kuhakikisha inaendelea kuunga Mkono juhudi za Wananchi kwa kuchangia ujenzi wa miradi iliyoanzishwa  na Wananchi sambamba na kuongeza mikopo kwa Vikundi vya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu vinavyotumia mikopo kwa tija na kurejesha kwa wakati. Aidha, Kamati imetoa rai kwa Viongozi wa Vitongoji, Vijiji, Kata na Chama katika ngazi ya Matawi na Kata kuwahamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya katika Zahanati ambazo hazina nyumba hali inayokwamisha utoaji wa huduma ya afya.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa