• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KAMPENI YA UTOAJI MSAADA WA KISHERIA NA UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA YAZINDULIWA MERU

Imewekwa: October 31st, 2022

Wananchi wa Halmashauri  ya Meru, Wilayani Arumeru wameishukuru Serikali ya awamu ya sita  ambapo kupitia  kampeni ya siku tatu ya utoaji msada wa kisheria na usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala inayowezeshwa na  wizara ya katiba na sheria  wameanza kunufaika .

Akizindua kampeni hiyo inayodumu kwa sikuu tatu, Mwl.James Mchembe ambaye ni katibu Tawala Wilaya ya Arumeru akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuhakikisha wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili wanasaidika kwa mujibu  wa  sheria ya utoaji msaada wa kisheria ya mwaka 2017 ambapo amewataka wananchi kujitokeza katika kampeni  inayoendelea katika Kata ya Ngarenanyuki ya utoaji msaada wa kisheria.

Mwl.Mchembe amewataka wataalumu katika kampeni hiyo kuwahudumia wananchi kwa weledi ili kampeni kuwa na tija "wasikilizeni wananchi ili muelewe  changamoto zao na kuwasaidia" amehimiza Mwl.Mchembe

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amesema kampeni hiyo ni fursa kwa wananchi kupata uelewa na msaada wa kisheria sambamba na kujua taratibu mbalimbali "katika kampeni hii mbali na uwepo wa  mabanda ya msaada wa kisheria pia uelewa na elimu ya masula mbalimbali inatolewa mfano tuna banda la Maendeleo ya Jamii  linaelimisha juu ya taratibu za kupata mkopo usio na riba unaotolewa na Halmashuri"amefafanua Makwinya

Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ngarenanyuki  Mhe.Aminiel Mungure kwa niaba ya wananchi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi  na kuomba Serikali kuendelea kutatua Migogoro ya Ardhi iliyopo ikiwemo ya ngazi za Mikoa na Wilaya.

Laurent Burilo  ambaye  amemwakilisha Msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa kisheria  Wizara ya Katiba na Sheria amesema  sheria ya utoaji msaada wa huduma za kisheria ya mwaka 2017 inalenga kutimiza azma ya serikali ya kuondoa migogora na kuendeleza amani ambapo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu na huduma bila gharama

Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria yenye kauli mbiu " *UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA HUPUNGUZA UADUI NA KUZUIA UMASKINI "* inaendelea katika Viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ngarenanyuki ambapo wananchi wanahudumiwa na wataalumu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  , Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, wataalum toka Halmashauri wadau toka TLS, LHRC,TAWLA nk,ambapo msaada wa kisheria juu ya masuala ya ardhi ,umiliki wa ardhi,ndoa na mirathi, ukatili wa kijinsia, vizazi na vifo nk unatolewa.

Baadhi ya picha za tukio


Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe

Diwani Kata ya Ngarenanyuki Mhe.Aminiel Mungure

Mwl.Zainabu Makwinya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru


Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini



Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI ANWANI ZA MAKAZI April 02, 2022
  • waliochaguliwa kwenye usaili wa tarehe 5 Aprili 2022 April 07, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA NAFASI YA KAZI KATIBU MAHSUSI DARAJA 111 May 26, 2022
  • MILIONI 50 ZA TOZO ZAKAMILISHA VYUMBA VINNE VYA MADARASA September 22, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • WASIOKAMILISHA MALIPO KUNYANG'ANYWA VIWANJA/MASHAMBA

    March 01, 2023
  • MHE.RAIS KUWASALIMIA WANANCHI WA ARUMERU

    March 04, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MERU LAIDHINISHA BAJETI BILIONI 54.1, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    February 21, 2023
  • Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akabidhi Ofisi

    February 01, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Salamu za sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2021.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa