Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Joseph Mabiti ameongoza kikao cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024.
Kikao hicho, kimehudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Taasisi, Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na wadau mbalimbali waliopo katika Halmashauri ya Meru.
Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Meru Sayi Manyanda amewasilisha vigezo vinavyotakiwa kufuatwa katika mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru.
Vile vile ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 utakimbizwa katika Mikoa yote 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ambapo Kwa mwaka 2024, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa wakati Taifa likiadhimisha miaka 25 ya kuondokewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Aidha, mwaka huu wa 2024 Taifa linaadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Miaka 60 ya Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu zianzishwe rasmi mwaka 1964.
Kauli Mbiu "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa