Madiwani Paulo Shango wa kata ya Kikwe, Peter Kessy wa kata King'ori na Bernard Kivondo wa Kata ya Majengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameapishwa kuwa madiwani rasmi wa Kata hizo katika mkutano wa baraza la madiwani.
Uapisho huo ni baada ya madiwani hao wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), kuibuka washindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata hizo uliofanyika tarehe 13 Octoba 2018.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Willy Njau amewakaribisha madiwani hao kwenye mkutano wa Baraza la Halmashauri kwa kuwakabidhi kitabu cha kanuni za kudumu za Halmashauri, kanuni za maadili ya madiwani, kabrasha la mkutano pamoja na vazi maalumu (joho).
Mkutano huo wa Baraza la Halmashauri umekamilika kwa siku ya kwanza katika ukumbi wa Halmashauri.
Aidha Uapisho huo ulioongozwa na Hakimu I. Nguma.
Mhe.Paulo Shango Diwani Kata ya Kikwe akila kiapo cha udiwani wakati wa Mkutano wa Baraza la Halmashauri.
Mhe.Peter Kessy Diwani Kata ya King'ori akila kiapo cha udiwani wakati wa Mkutanowa Baraza la Halmashauri.
Mhe.Benard Kivondo Diwani Kata ya Majengo akila kiapo cha udiwani wakati wa Mkutanowa Baraza la Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru Mhe.Will Njau akimkabidhi Mhe.Paulo Shango Diwani Kata ya Kikwe kanuni za kudumu za Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru Mhe.Will Njau akimkabidhi Mhe.Benard Kivondo Diwani Kata ya Majengo kanuni za kudumu za Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa zoezi la kuapishwa madiwani 3.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa kuapisha madiwani 3.
Wakuu wa idara ,viongozi wa vyama vya siasa na wageni wakifuatilia zoezi la kuapishwa madiwani 3.
Wakuu wa idara,viongozi wa vyama vya siasa na wageni wakifuatilia zoezi la uapishaji.
Viongozi wa vyama vya siasa, wageni na wananchi wakifuatilia zoezi la uapishaji.
Viongozi wa vyama vya siasa, wageni na wananchi wakifuatilia zoezi la uapishaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa