Viongozi wa Vyama vya Siasa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wapatiwa Mafunzo dhidi ya Sheria kanuni na taratibu za Vyama vya Siasa Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 Mwaka huu.
Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Makao Makuu Dodoma Emmanuel David Msengi amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa kufuata kanuni na taratibu za Vyama vya Siasa kama Sheria ya Vyama vya Siasa Sura na.258 inavyohitaji.
Msengi amesisitiza Zaidi Juu ya Vitendo vinavyokatazwa Kwa Vyama vya Siasa kuzingatiwa Zaidi hasa katika kipindi hichi cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuendelea kudumisha Amani na kujikinga kutokupatiwa adhabu Kwa Chama kitakacho kwenda kinyume na Sheria zilizowekwa
Wajumbe wa Mafunzo hayo ni Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Siasa kinachotambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri Kwa ngazi ya Serikali.
Aidha msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ameishukuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Kwa Mafunzo haya waliyo yatoa kwani yataendelea kuleta uelewa Kwa viongozi wa vyama vya Siasa na kuleta umoja wa kimaendeleo Kwa Jamii zinazo wazunguka
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa