Katika kutekeleza Ilani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ibara ya 52,Serikali kwa kipindi cha miaka 3 imetoa Shilingi Bilioni 4 kwaajili ya Elimu bila malipo ambapo kwa wastani kila mwezi Serikali hutoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru zaidiya shilingi milioni 60 kugharamia elimu bila malipo kwa Shule za Msingi.Aidha, zaidi ya shilingi milioni 55 hutolewa kugharamia elimu kwa Shule za Sekondari.
MATOKEO YA ELIMU BURE KATIKA HALMASHAURI YA MERU.Kumekuwa na ongezeko la Wanafunzi katika Shule za Sekondari na Msingi ambapo idadi ya Wanafunzi waliojiunga Sekondari kidato cha kwanza mwaka 2015 ilikuwa 2622 kabla ya utekelezaji wa Elimu bila malipo na mwaka 2019 idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 4924. Kwa upande wa Shule za msingi Idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la awali imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka 6809 Mwaka 2015, 7052 mwaka 2017 ,7196 mwaka 2018 na 7700 mwaka 2019.Elimu bila malipo imeongeza asilimia ya ufaulu ambapo asilimia ya ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa kuhitimu kidato cha sita mwaka 2016 ilikuwa 92.06%,na Mwaka 2019 imefika 99.7%, Katika Mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne,mwaka 2015 asilimia ya ufaulu ilikuwa 89.16% na mwaka 2018 ilifikia 96.92%,Mtihani wa upimaji kidato cha pili mwaka 2015 asilimia ya ufaulu ilikuwa 89.16% na mwaka 2018 ilikuwa 96.92% na katika Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi darasa la saba (vii), mwaka 2015 ilikuwa 67.6% na mwaka 2018 ilifikia 86.6%.
ELIMU BILA MALIPO IMEENDA SAMBAMBA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU.
Serikali kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (EP4R)imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne na vyoo vya matundu 6 katika Shule ya Msingi wa maboma 16 (vyumba vya madarasa) katika shule za Msingi 16. Tanzanite na Kisimiri juu,pamoja na ukamilishaji.
MCHANGO WA HALMASHAURI
Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kupitia Mapato yake ya ndani imetoa zaidi ya milioni 63 kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya Elimu ikiwani ununuzi wabati 384, mifuko ya Saruji 640 na viti na meza 600.
MCHANGO WA JAMIIMCHANGO WA JAMII
Elimu bila malipo imekuwa kichocheo kwa wazazi ambapo wamehamasika kuchangia zaidi ya milioni 357 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule za Sekondari.
Vyumba Viwili vya Madarasa Shule ya Msingi Tanzanite
vyoo vya matundu 6 katika Shule ya Msingi Tanzanite
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa