MCHONGO NI AFYA ZINGATIA UNACHOKULA
Ni kauli Mbiu inayosindikiza Siku ya Afya Kitaifa ambapo Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeadhimishwa katika Kata ya Nkoanrua huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ametoa pongezi kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kwani jumla ya watoto 40,504 sawa na asilimia 98.6 wamepimwa hali ya lishe kwa kigezo cha uzito na umri na kuonekana swala la afya zao lipo vizuri kwa kiwango kikubwa lakini pia amewasisitiza wakina mama kuachana na Mila potofu hasa kwenye swala la afya dhidi ya watoto na kuwataka kufuata yale wanayoshauriwa na wataalamu wa Afya.
lakini pia amewataka wakina Baba kuwa msaada wa kwanza kwa wakina mama pindi wanapokuwa katika majukumu ya malezi ya watoto hivyo wakina Baba kuacha ubwenyenye na kuwa mstari wa mbele kusaidia majukumu ya nyumbani ili kumpa nafasi mama na muda wa kupumzika ikiwa ni pamoja na kula vizuri ili aweze kutengeza Chakula chakutosha kwa Mtoto.
Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kupitia hafla hiyo kwamba klabu za lishe zianzishwe mara moja mashuleni na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanakula chakula pindi wanapokuwa shuleni na kama kuna mzazi atashindwa kumchangia Mtoto wake kupata chakula basi anastahili kupelekwa mahakamani kwani hatimizi wajibu wake kama mzazi na anavunja Sheria na haki za Mtoto.
Mwisho Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kupitia Vyama vyao vya Siasa kushiriki Uchaguzi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa kwani atakaeshindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa