Halmashauri ya Wilaya ya Meru chini ya Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Zainabu J. Makwinya imetoa mrejesho wa fedha zilizotumika za mapato ya Ndani kwa kipindi cha Miaka Mitatu kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Katika Halmashauri hiyo.
Katika Kikao Kazi cha Watendaji wa Kata na Vijiji Mkurugenzi Makwinya ametoa mrejesho wa kile kilichofanywa na Halmashauri na kuelezea kuwa shilingi Bilioni 1,819,061,767.00 zimetolewa katika Mapato ya Ndani kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwa upande wa Elimu Sekondari, Elimu Msingi na Afya.
Makwinya ameleeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri ya Meru kama Halmashauri nyingine imenufaika kwa fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 21.5 zimetolewa kwa Sekta ya Elimu Sekondari, Elimu Msingi , Afya na Utawala.
Ameleeza kuwa lengo la kutoa tathmini hiyo ni kuona Serikali imesaidia nini na Halmashauri imefanya nini ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na kufikia Bilioni 10 ukilinganisha na ukusanyaji wa sasa wa Bilioni 6.1 kutoka ukusanyaji wa zamani wa Bilioni 3.6 wa miaka mitatu ya nyuma ambao ni ongezeko la asilimia 77% za ukusanyaji wa mapato.
Katika Kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia ukusanyaji wa Mapato katika maeneo yao na kujipima katika utendaji kazi kwa kipindi cha Miaka 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021, 2021/2022 na 2022/2023 ili kuweza kufikia makusanyo ya sh. Bilioni 10.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda katika kikao kazi hicho ametoka pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa malezi mazuri kwa watumishi anaowaongoza lakini pia, kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Katika kikao hicho Wakuu wa Idara na MÃ afisa wa Ulinzi na Usalama walipata nafasi ya kutoa mada mbalimbali zinazohusiana na utekelezaji wa shughuli za Halmashauri na masuala ya kijamii
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa