• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MERU, ELIMU YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA YATOLEWA KWA VIONGOZI WA DINI , VIONGOZI WA KIJAMII NA WADAU WA AFYA

Imewekwa: October 17th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa wito kwa viongozi wa Dini ,Viongozi wa kijamii na wadau wengine katika sekta ya afya kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa Ebola ambao mlipuko wa ugonjwa huo umeripotiwa nchi Jirani ya Uganda.

Mhe.Ruyango amesema hayo wakati wa Kikao cha kamati ya Afya ya Msingi (PHC) ngazi ya Wilaya Halmashauri  ya Wilaya ya Meru ambapo amesema Kutokana na muingiliano kati ya nchi na nchi ,hatuna budi kuchukua tahadhari  kwani  kuna uwezekano wa ugonjwa huo kuenea  .

Akiwasilisha Mada ya Ugonjwa wa Ebola, Dkt.Emmanuel Kinayi amesema Ugonjwa wa Ebola hauna tiba maalum wala chanjo kwani Mgonjwa hupewa tiba saidizi kulingana na dalili alizonazo , kama vile Tiba ya kushusha homa na maumivu, Kuongezewa damu na maji mwilini, Tiba lishe.

Dkt. Kinayi amesema ugonjwa wa Ebola unasababishwa na virusi vya Ebola ambavyo hubebwa na wanyama kama vile Nyani,Sokwe,Gorilla,Kima ,Popo ,Swala swala  ambapo husambazwa kutoka  kwa wanyama hao kwenda kwa binadamu  kwa kula nyama,mizoga  au kuwagusa.

Vilevile Dkt.Kinayi amesema ugonjwa wa  Ebola  huenezwa kupitia  sehemu za wazi za mwili kama vile pua, masikio na macho ambapo humuathiri binadamu na wanyawa endapo vimelea vitaingia katika mzunguko wa damu . 

Mkuu wa Idara ya Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt.Focus Maneno ametoa wito kwa jamii kujikinga na  ugonjwa wa Ebola  kwa kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana, kutokugusa damu , matapishi , mkojo ,kinyesi , kamasi , mate , machozi na maji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu, kutokugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola, kuepuka kutumia nguo , shuka , blanketi , kitanda na godoro za mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu, kunawa  mikono kwa maji tiririka  na sabuni mara kwa mara,kuepuka kugusa wanyama kama vile popo , nyani , sokwe , tumbili na swala au mizoa ya wanyama

Dkt.Maneno amesema endapo mtu atakuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo huonekana  kati ya siku 2 hadi 21 baada ya mtu  kupata maambukizi kutoa taatifa mapema kwa uongozi ambapo ametaja dalili hizo kuwa ni pamoja kuwa na homa kali ya ghafla,maumivu ya kichwa,maumivu ya mwili , misuli na viungo,
Kuharisha (kunakoweza kuambatana na damu),Kutapika (kunakoweza kuambatana na damu),Vipele mwilini,
Kuvia damu chini ya ngozi au kutokwa na damu puani , mdomoni , machoni na masikioni.


Aidha amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola aliyegundulika na hivyo ameomba wadau wote kushirikiana na sekta/Idara ya Afya ili kufanya maandalizi muhimu ya kukabiliana na mlipuko wa magonjwa ikiwemo Ebola.

 *UGONJWA WA EBOLA HAINA TIBA ,TUJIKINGE KWA KUCHUKUA TAHADHARI*

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza wakati wa kikao.

Viongozi wakisikiliza taarifa ya  ugonjwa wa Ebola.

Viongozi wa Dini ,Viongozi wa kijamii ,na wataalum wakati wa kikao




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa