Na Annamaria Makweba
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Voice of Youth Tanzania (VOYOTA) imekabidhi Mapipa Sita ya kuhifadhi Taka ngumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Vicent Uhega amekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda katika Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri hiyo.
Katika Makabidhiano hayo Mhe. Kaganda ametoa shukrani kwa taasisi hiyo kwa mchango wao katika kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira, aidha ameshauri mapipa hayo yakawekwe karibu na vituo vya Daladala na waendesha bodaboda ili waweze kusaidia katika suala la ulizi wa mapipa hayo sambamba na utunzaji wa mazingira katika maeneo hayo.
Mapipa yaliyokabidhiwa yameambatana na jumbe mbalimbali za kupinga masuala la ukatili kwa leo la kuendelea kutoa elimu kwa jamii kutokomeza masuala na kupinga Ukātili.
Kati ya jumbe zilizoandikwa kwenye mapipa hayo ni pamoja na " Usimdunde Mkeo dunda Kitenesi" na " Ukatili wa kijinsia ni kinyume na Haki za Binadamu tokomeza ukatili kwa jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa