• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Mkoa wa Arusha Wazindua kampeni ya NILINDE MIMI NA MAMA YANGU TUISHI.

Imewekwa: February 22nd, 2021

Kampeni ya NILINDE MIMI NA MAMA YANGU TUISHI  inayolenga kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga imezinduliwa Mkoani Arusha wakati wa kikao cha kujadili vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu maalumu Patandi ,kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru..

Akizindua kampeni hiyo   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa,amesema kampeni hiyo ni  miongoni mwa mikakati ya Mkoa wa Arusha  kudhibiti vifo vitokanavyo na  uzazi na vifo vya watoto wachanga.

Aidha, Muro ametoa wito kwa wahudumu wa afya,watendaji wote wa Serikali na jamilii kutekeleza wajibu wao na kushirikiana ili  kuhakikisha wanapunguza au kumaliza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga "hatutegemei  kuwa na vifo vya  mama au watoto ambavyo vimesababisha na uzembe''amesisitiza Muro.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha   Dkt. Wedson Sichalwe amesema  kikao hicho  ni kwa mujibu wa matakwa ya kisera ambapo hufanyika kila robo ya mwaka kikilenga kupunguza kasi ya vifo hivyo , japo  takwimu zinaonesha mafanikio ya kupungua kwa vifo ambapo   mwaka 2019 kulikuwa na vifo 67  na mwaka 2020 vilipungua kufikia 46 bado jitihada mahsusi zinahitajika.

Ndg.Emmanuel Mkongo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema kunaumuhimu mkubwa kutoa elimu kwa jamii juu ya  dalili hatarishi kwani jamii ina kipaumbele kupunguza vifo kwa kuwawahisha wajawazito kuwahi hospitali,kuhudhuria cliniki pamoja na kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkongo amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani itajenga kituo cha afya katika Kata ya Maroroni kitakacho gharimu Shilingi Milioni 400 ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuzuia vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Kikao hicho kilichojumuisha timu za usimamizi wa afya ngazi ya  Mkoa ,Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Meru kinatarajiwa kuendelea kwa siku nne ikiwa ni pamoja na wajumbe  kufanya usimamizi shirikishi katika halmashauri ya Meru.



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza .

Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha   Dkt. Wedson Sichalwe akizungumza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza.


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa