Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewataka Watumishi wa Halmashauri hiyo kuchapa kazi kwa uadilifu, Uaminifu na ushirikiano ili utendaji wao kuwa na tija kwenye maendeleo ya Halmashauri ya Meru.
Makwinya amesema hayo wakati wa kikao Kazi na wakuu wa Idarana Vitengo ambapo amebainisha kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato kuwa kipaumbele chake hivyo amewataka wakuu hao wa Idara kuhakikisha mapato yanakusanywa katika Kata wanazozilea kwa kiwango stahili kwa kudhibiti mianya ya upotevu _"Swala la ukusanyaji mapato ni la kila mmoja wetu na sio Idara ya fedha Pekee" amehimiza Mwl.Makwinya
Aidha, Makwinya amewataka wakuu hao wa Idara kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa Wananchi kwa kujikita katika mkataba wa huduma kwa wateja ili kutatua kero na kuondoa malalamiko.
Akihitimisha Makwinya amefafanua kuwa uadilifu ni Msingi wa haki ambapo amewataka Watumishi kuwa na Umoja, Kushirikiana, Kuheshimiana na kutenda haki pahala pa Kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya
Ndg.Hamson Mrema Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii akitoa neno la ukaribisho
Mkuu wa Idara,Kaimu wakuu wa Idara na Mratibu w TASAF wakati wa kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa