Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amezindua rasmi maadhimisho ya wiki ya mazingira katika halmashauri hiyo na kuongoza wananchi kukufanya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuokota taka kwenye maeneo ya wazi, Makazi, maeneo ya biashara na barabarani .
Awali, akizindua maadhimisho hayo ya wiki ya mazingira ambayo ni kuanzia leo tarehe 01 hadi 5 Juni 2022, yenye kauli mbiu *"Tanzania ni moja, Tutuze mazingira*"
,Mwl.Makwinya ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kufanya usafi kwenye makazi yao, maeneo ya biashara, maeneo ya wazi, mitaro ya maji, barabarani nk "ushiriki wa kila mmoja huleta tija kwenye maadhimisho haya, mazingira masafi ni salama kwetu sote" amehimiza Makwinya.
Baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wameonesha kuvutiwa na namna wadau na viongozi wamekuwa mstari wa mbele kwenye maadhimisho hayo "tumefurahi kuwaona viongozi wakishirikiana nasi kufanya usafi hii imetuhamasisha sana na sisi tunawaahidi kushiriki ipasavyo kwenye maadhimisho haya "amesema Neema James mfanyabiashara wa Leganga ,Usa -River.
Aidha, maadhimisho hayo yataendelea kwa siku tano tarehe 01 hadi 05 Juni 2022 ambapo wananchi wanatakiwa Kufanya Usafi kwenye maeneo yao, kufyeka nyasi, majani na vichaka kwenye maeneo ya makazi, maeneo ya biashara na maeneo ya umma, kwenye barabara, masoko pamoja na kuzibua mifereji ya maji.
Pia.shughuli za Kupanda miti kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya makazi, maeneo ya biashara, mashuleni,maeneo ya wazi na Taasisi mbalimbali zitafanyika
Vilevile , katika kilele cha maadhimisho haya tarehe 05 Juni 2022 kutakuwa na kongamano la wadau wa mazingira litakalofanyika eneo la mbele la Halmashauri kuanzia saa 2:00 asubuhi na Wananchi wote mnakaribishwa.
Uzinduzi wa wiki ya mazingira kitaifa umefanyika Jijini Dodoma na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru uzinduzi umefanyika katika makao makuu, wadau walioshitiki ni Wananchi , Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Twice foundation, Hakiki Ndoto zako organization, Usa River Malihali Club, Duluti Green Foundation, Dunia Salama Foundation, Kilimanjaro Experts, Joboritunity, Life for Change, Ngare sero Mountain Lodge, Bodi ya Maji Bonde la Pangani pamoja na wananchi na watumishi Mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa