SHIWARA SACCOS LTD Wamefanya mkutano Mkuu ambao umeambatana na Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Chama hicho huku Mgeni Rasmi akiwa Ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha Robert George.
Mrajis amekipongeza Chama cha Ushirika cha SHIWARA Kwa kazi nzuri wanayoifanya na hata kufikia Kujenga Ofisi kubwa itakayowasaidia kuendesha shughuli zao za kimaendeleo na kuwataka waendelee kuwa na Umoja mshikamano Kwa manufaa mapana ya SACCOS Yao. Pia ametoa Elimu kuhusu saccos na kuonesha umuhimu wa wanachama hao kuwa kwenye SACCOS.
Aidha Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake kwenye Chama hicho Asoraeli Nanyaro amewahasa wanachama kuendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi watakaopatikana kama ushirikiano walio uonyesha kwake na hata kufikia mafanikio ya kuwa Chama Bora cha Ushirika cha huduma kwa jamii kwa mwaka 2023 katika maonyesho ya siku ya Ushikia wa Akiba na Mikopo (ICUD) yaliyofanyika jijini Mwanza na kushinda Nafasi hiyo.
Wananchi Mbalimbali wameonyesha kupendezwa na Mpango huu wa Vyama vya Ushirika Kwa manufaa mbalimbali wanapokutana nayo ikiwemo Upatikanaji wa Mikopo yenye Riba nafuu.
Chama cha Ushirika SHIWARA SACCOS LTD kimetimiza Miaka 22 Tangu kuanzishwa kwake kikiwa na wanachama 841 mpaka sasa huku kikiinua Wananchi wa Kata ya Songoro kwenye Mikopo ya Elimu, Biashara, Kilimo na Uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa