Halmashauri ya Wilaya ya Meru Tarehe 02.10.2023 imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya Kwanza Julai hadi Septemba kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwa ni kuwasilisha taarifa kutoka katika Kata 26 zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji za Kata kwa kipindi cha Julai - Septemba 2023/2024 na kueleza hali ya utoaji wa hudumu za kijamii kwa ujumla na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Masuala ya Elimu katika Kata, hali ya shughuli za kiuchumi, mafanikio, changamoto na utatuzi wake, utunzaj wa mazingira na vyanzo vya majl pamoja na mipango ya baadae.
Utaratibu wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika Mkutano wa Halmashauri ni kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halmashauri za mwaka 2014 chini ya kanuni ndogo ya 3(1).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa