• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MKUU WA MKOA WA ARUSHA APONGEZA WAOMAN KUCHIMBA KISIMA MERU

Imewekwa: May 17th, 2022

Zaidi ya wanafunzi 2,500 katika shule tatu za Sekondari na shule mbili za Msingi za Halmashauri ya Meru,Wilayani  Arumeru  wamenufaika na huduma ya maji  baada ya kuchimbiwa visima na wadau wa Maendeleo kutoka nchini Oman.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amempongeza Ndg.Nasr Masaoud Aljahadhamy  kutoka Oman pamoja na wenzake wa kundi Sogozi la Tuelekezane Peponi kwa kuchimba visima vinne vya  maji katika Shule za  Sekondari patandi Maalum, Shule ya Sekondari Makiba,Shule ya Sekondari Kitefu ,Shule ya msingi Miembeni pamoja na kuzibua kisima kimoja  katika shule  ya msingi Patandi.

Aidha,Mhe.Mongela amekabidhi zawadi  za vikombe na vyeti vya kutambua mchango wa wadau hao  kuunga mkono juhudi za Serikali katika uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya miundombinu   ya maji mashuleni.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ambaye Halmashauri yake imenufaika, amesema chimbuko la kupata wadau hao ni  kupitia maadhimisho ya siku  ya  wanawake ambapo  walichanga zaidi ya  Milioni 3.6 kwa ajili ya  wanafunzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum na shule ya Msingi Patandi ambapo shule hizi zinawanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Aidha Mwl.Makwinya amewashukuru Sheikh Ayubu Hussein,Shahidu Ally na Hassan Fazal PCP  kwani siku wanawake wa Meru wakikabidhi mchango wao katika  shule ya Sekondari Patandi Maalum walikutana na  Masheik hao wakiwasilisha  sadaka ya Iftar na Daku kwa wanafunzi  ambapo waliahidi kuwakutanisha na  Ndg.Nasr Masaoud Aljahadhamy kutoka nchini Oman

"Tunawashukuru wadau wa Maendeleo kutoka nchini Oman kwa moyo wao wa kutuchimbia visima pia wametuahidi kutuletea vifaa kadhaa kama printa vitimwendo, Mablanket n.k. hivyo kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kwani serikali imewekeza fedha nyingi sana katika miundombinu ya shule"

Kwa Upande wake Nasr Masaoud Aljahadhamy  amesema toka mwaka 2016  wameshachimba visima 56  hapa nchini na wataendelea kusaidia katika zoezi hilo kwa kushirikiana na serikali katika kusaidia  kusogeza mbele maendeleo

Awali, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Meru  Emmy Mfuru amesema kupatikana kwa huduma hiyo  ya maji ni muhimu sana haswa kwa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum kwani swala la usafi na mazingira hutegemea maji ambapo amefafanua upatikanaji huo wa maji  ni chachu ya  uboreshaji mazingira ya kujifunzia na kufundishia .

Nae Mdau wa Maendeleo  Sheikh Ayoub Hassan  ameishukuru  serikali kwa kuendelea kushirikiana  na wadau mbalimbali wakiwemo  viongozi wa dini katika kuwaletea wananchi maendeleo  maendeleo.

.Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela akikabidhi kikombe cha kutambua mchango kwa Nasr Masaoud Aljahadhamy toka Nchini Oman

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela akikabidhi cheti cha kutambua mchango kwa Sheik Ayoubu Hussein  toka hapa Nchini ,Pembeni Ni mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya.


Afisa Elimu Sekondari Emmy Mfuru 

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa