Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jonathani Kiama amewataka Wasimamizi wa Vituo vya kupiga kura na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupiga kura katika Vijiji vya Ngongongare, Miririny na Imbaseni kuzingatia
Kiama amesisitiza hayo wakati wa semina elekezi kwa wasimamizi hao wa Vituo vya kupiga kura pamoja na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupiga kura wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa,ambapo wamekula kiapo cha kutunza siri ,utii na uadilifu
Kiama amesema uchaguzi utafanyika kwenye Vijiji vitatu tuu kati ya Vijiji 90 vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru,hii ni kutokana na wagombea wengi kukosa sifa wakati wa zoezi lakuteua wagombea pia baadhi ya wagombea kujitoa kwenye uchaguzi,"nitoe wito kwa Wananchi wa Vijiji vya Ngongongare, Miririnyi na Imbaseni kujitokeza kupiga kura kumchagua kiongozi ataklayewaletea maendeleo.'amesisitiza Kiama.
Aidha vijiji vitakavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 24 Novemba 2019 ni kijijji cha Ngongongare, Miririnyi na Imbaseni na Vijiji vingine 87 vyilivyobaki havitakuwa na uchaguzi Kutokana na Wagombea wake kupita bila kupingwa baada ya Wananchi wengi waliosimamishwa na Vyama vyao vya kukosa sifa wakati wa zoezi la uteuzi na wengine kujito kwenye Uchaguzi.
Vituo vya kupiga Kura vitafunguliwa saa 2:00 kamili Asubuhi na kufungwa saa 10:00 kamili jioni
Baadhi ya picha za tukio.
Wasimamizi hao wa Vituo vya kupiga kura pamoja na Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupiga kura wa Uchaguzi wa kata ya LE
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa