Mgombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi, (C.C.M) Ndg.John Pallango atangazwa rasmi kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, msimamizi wa uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo amemtangaza John D. Pallangyo kupita bila kupingwa kwenye Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimboni humo.
Mkongo amesema kuwa toka zoezi la kuchukua fomu lianze tarehe April 15 Aprili mwaka 2019, jumla ya wagombea 11 walijitokeza kuchukua fomu lakini hadi kufikia 10:00 jioni ya leo wagombea watatu ambao ni Antonia Ndosi (DP),George Nashoni (CUF) Msifuni Mwaja (TL) walishindwa kurudishwa fomu.
Aidha Mkongo ameeleza kuwa wagombea wengine saba ambao ni Mohamed Kitundu (SAU),Juma Ntajera (ADA- TADEA), Tulisabya Lwitakubi (UNDP),Mgina Mustafa (AAFP) Rashid Mkama (NRA),Cosmas Kavishe(NCCR) Mageuzi, Saimon Ngilisho(Demokrasia Makini) wa vyama vya upinzani walirejesha fomu lakini wakati wa ukaguzi NEC ilibaini fomu zao kuwa na dosari mbalimbali zilizosababisha kuenguliwa kwenye mchakato huo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kupita bila kupingwa Ndg.John Pallangyo ameishukuru NEC kwa kufanya kazi yake kwa uadilifu pamoja na mwenyekiti wa CCM taifa Rais John Magufuli kwa kupitisha jina lake kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM ili apeperushe bendera ya CCM.
Aidha Pallangyo amewahidi wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki kuwa atashirikiana nao kutatua kero walizo nazo mara baada ya kuapishwa.
Aidha wagombea saba ambao hawakukidhi vigezo vya NEC,wamekiri kuridhika na matokeo ya uteuzi wa Ndg. John Pallangyo na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha.
Naye mshili mkuu wa viongozi wa mila na tamaduni za Meru Ezron Summary alimuomba Mbunge huyo mteule kushirikina na wananchi wa Meru na kuwaletea maendeleo.
Ikumbukwe kuwa zoezi la urejeshaji fomu za kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki lilianza tarehe 15 Aprili 2019 na kuhitimishwa leo Tarehe 19 Aprili 2019 saa 10:00 kamili jioni.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa