Wanakijiji wa Kijiji cha Imbaseni wamezingatia usemi "Maendeleo ya Mtu ni Mtu mwenyewe" kwa kushiriki kwa michango na nguvu zao kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho , Afisa Mtendaji wa Kjiji hicho Glory Urio amesema Mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho uliibuliwa kwenye Mkutano wa Kijiji ambapo Wananchi walipitisha mchango kwa awamu ya kwanza utakao tumika kujenga msingi na kumwaga jamvi jambo ambalo linatekelezwa kwa sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Christopher J. Kazeri alipotembelea Mradi huo amewapongeza Wananchi hao kwa kuendana na Azma ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuachana na Siasa na kufanya kazi za Maendeleo kwani baada ya wataalamu wake wa ujenzi kufika siku ya jana naye amefika ili kuona kazi inayoendelea na pia kuona ni kwa jinsi gani Halmashauri itachangia.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa