• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

JUKWAA LA USHIRIKA ARUMERU LATOA SHUKA 30 KWAAJILI YA VITUO VYA AFYA.

Imewekwa: August 31st, 2018

Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru,Mch. Anael Nassari wakati wa uzinduzi wa Jukwaa  la Wilaya la Ushirika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Meru amemkabidhi mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jerry Muro Shuka 30 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa kwenye vituo vya Afya.

Mchungaji Nassari ameeleza kuwa  Vyama vya Ushirika mbali na kuwajengea uwezo wa kujikomboa kiuchumi pia kati ya misingi saba ya Ushirika,mmojawapo ni kuijali jamii hivyo kuna baadhi ya Vyama vilishatoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule lakini kupitia Jukwaa  hilo wameshiriki kuboresha huduma za afya kwa kujitolea shuka hizo.

Akipokea mchango wa shuka hizo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amepongeza juhudi za Ushirika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za Afya ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100% kwenye wilaya hiyo.

Mhe. Muro amesema serikali ya awamu ya tano inahakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya ampapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018  wilaya hiyo imepewa  bilioni moja na Milioni 400 kwa ajili ya kuboresha vituo vya Afya  vitatu, Usa – River, Nduruma na Mbuyuni .

Mh. Jerry Muro amekabidhi shuka hizo kwa Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara kwa ajili ya matumizi katika  kituo cha Afya Usa-River.

Kituo cha Afya Usa-River Kilichopo Halmashauri ya Meru  kiliboreshwa kwa milioni 500 huku vituo  vya Afya  viwili  Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambavyo ni Nduruma  kuboreshwa kwa milioni 500 na Kituo cha Afya Mbuyuni mwishoni mwa mwaka wa fedha 2017/2018 kimepokea milioni 400 na uboreshaaji unaendelea.

Uboreshaji  wa Vituo vya Afya hufanyika kwa  ujenzi  wa majengo ya kisasa  ya wodi ya mama na mtoto, upasuaji, maabara ,nyumba za watumishi pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti pia kukarabati majengo yaliyopo.

Uundaji wa Majukwaa ya ushirika ngazi ya Mkoa na Wilaya hutoa  fursa kwa Vyama vya Ushirika kukutana kubadilishana mawazo, kupeana uzoefu, kujadili changamoto zinazoukabili Ushirika na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo.

PICHA ZA TUKIO.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro na Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Wilayani Arumeru Mch.E Nassari wakati wa makabithiano ya shuka kwaajili ya vituo vya Afya.

 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara  akipokea shuka toka Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akiwashukuru wanaushirika kwa kuungamkono Uboreshaji wa Huduma za Afya Wilayani hapo.

Mkuu wa Kitengo cha  Ushirika  Halmashauri ya Meru  Mkumbwa Mussa (kulia ) pembeni yake  ni Afisa ushirika  kwenye Halmashauri ya Meru Neema Mundo.

Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.

Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.

Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.

Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa