Vijana 26 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamekabidhiwa vocha za ruzuku ya ada itakayowawezesha kupata mafunzo ya ufundi bila malipo kwenye vyuo mbalimbali Nchini.
Afisa vijana wa Halmashauri ya Meru Ndg.Lily A. Msemo ameeleza vijana 42 wa halmashauri hiyo walikidhi vigezo vya kupata vocha ya ruzuku ya ada ambapo leo vijana 26 wamekabidhiwa vocha hizo na waliobaki watakabidhiwa pindi watakapo jitokeza.
Meneja wa bodi ya mikopo kanda ya kaskazini Patrick shoo amefafanua kuwa utoaji wa Vocha za ruzuku ya ada ni Azma ya serikali kuwawezesha vijana kupata ujuzi ili kuweza kujiajiri wenyewe, kuajiriwa,kujikimu kimaisha pia kutoa mchango kwenye jamiii na Taifa kwenye kuelekea uchumi wa kati.
Ndg.Shoo amefafanua kuwa kijana atapata Vocha ya ruzuku ya ada endapo atakua na sifa zifuatazo ,kuwa raia wa Tanzania,umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 30 na awe anatoka kwenye familia duni pia mefafanua zoezi hilo la utoaji vocha ya ruzuku ya ada ni la majaribio ambapo limeanza kwa mikoa ya Arusha,Dodoma,Manyara na Singida
Aidha Shoo ameeleza Vijana wa 179 wa Arusha ni miongoni mwa vijana 1074 walionufaika katika mikoa iliyotajwa na vijana wengine ambao fomu zao za maombi zilikuwa na mapungufu mbalimbali watapatiwa vocha zao baada ya kurekebisha mapungufu hayo pia amefafanua zaidi ya vijana 32,000 watanufaika na mpango huo Nchi nzima ambao umelenga kuwaweza vijana kupata ujuzi katika maeneo ya Ujenzi,Nishati,Kilimo,utalii na ukarimu ,usafirishaji na lojistiki pamoja na teknolojia ya mawasiliano na habari.
ikumbukwe kuwa zoezi la utoaji wa vocha ya ruzuku ya ada kwa vijana linafanyika kwa awamu hivyo vijana wengine bado wananafasi ya kupata fursa hii zaidi ya vijana 300 watanufaika.
Picha za tukio.
Meneja wa bodi ya mikopo kanda ya kaskazini Patrick shoo akimkabidhi Dickison T. Pallangyo vocha ya ruzuku ya ada kwa
Meneja wa bodi ya mikopo kanda ya kaskazini Patrick shoo akimkabidhi Evenlight vocha ya ruzuku ya ada kwa
picha ya pamoja (wa pili kushoto) Afisa vijana wa Halmashauri ya Meru Ndg.Lily A. Msemo ,Meneja wa bodi ya mikopo kanda ya Kaskazini na vijana wakionesha vocha za ruzuku ya ada walizo kabithiwa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa