Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel Mkongo wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa taarifa za wanafunzi PReMS kwa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na binafsi yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkongo amesema matumizi ya mfumo yatarahisisha utendaji ambapo muda uliokuwa unatumika kujaza taarifa na kuwasilisha Wilayani utatumika kuongeza kiwango cha taaluma.
Aidha, Mkongo amesisitiza ujazaji wa taarifa katika mfumo ili kuwa na kumbukumbu zitakazo tumika kwa maswala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhamisho wa wanafunzi.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo Mwl.Emmy Mfuru amewasisitiza walimu hao kuhakikisha wanalinda Nywila za kuingia katika mfumo huo ambao unamtaka Mkuu wa Shule na Mwalimu wa Taaluma pekee kuingia na kutumia. Aidha, Mwl.Emmy Mfuru ametoa wito kwa Wakuu Shule kuhakikisha wanafanya kazi kwa wakati kwenye mfumo huo "hakikisheni uamisho wa wanafunzi unachukua siku chache"amesisitiza Afisa elimu.
Mafunzo hayo ya matumizi ya mfumo wa taarifa za Wanafunzi wa Shule za sekondari yamehusisha walimu Wakuu na Walimu wa taaluma kutoka shule za Sekondari za Serikali 35 na Shule za sekondari za binafsi 31 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel Mkongo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Walimu wa Taluma wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel Mkongo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Emmy Mfuru .
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReMS.
Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa mafunzo ya mfumo wa PReM.

Mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo wa PReMS Ndugu Imani Baharia akitoa maelekezo kwa wanasemina namna ya kutumia mfumo wa PReMS
Afisa Taaluma Mwl.Neema mbiyo akiwasikiliza Wakuu wa shule wakati wa mafinzo
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa