Wito watolewa kwa Walengwa wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Meru kutumia fedha zinazotolewa na TASAF kama ilivyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi .
Wito huo umetolewaa na BW.Christopher Pallangyo ambaye ni mlengwa wa TASAF toka kijiji Cha Nkoaranga ambaye ameweza kutumia kiasi cha fedha anazopokea kutoka TASAF kununua na kupanda Miche 200 ya Kahawa.
Pallangyo amesema mbali na kiasi anachopokea kuwa kidogo (Shilingi elfu 20) aliweza kukusanya na kununua Miche hiyo pamoja na ameweza kujenga nyumba ambayo haijakamilika ,ameweza kununua ndama pamoja na kupata mahitaji yake madogo madogo.
Pallangyo ameishukuru Serikali na kuiomba kuendelea kusaidia Kaya sisizo na uwezo pamoja kuongeza kiasi cha fedha zinazotolewa kwa walengwa ili kuharakisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi .
Aidha,Serikali imetoa zaidi ya Milioni 184 kama malipo kwa Walengwa wa TASAF kipindi cha Miezi 2 (Machi na Aprili).Fedha hizi ni malipo kwa Kaya za walengwa 5083 TASAF toka Vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Kwa sasa zoezi la malipo linaendelea kwa muda wa siku 7.
Ikumbukwe kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, mpango wa kunusuru Kaya maskini (TASAF) ulianza Mwaka 2014 na malipo kwa Walengwa yalianza kutolewa Mwaka 2015.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa