Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Chembe wakati wa kikao cha ushauri cha Wilaya hiyo amewakumbusha watumishi wa Serikali Wilayani humo kuzingatia maadili ya utumishi wao katika kutekeleza majukumu yao.
Mwl.Chembe ameongeza kuwa mtumishi wa Umma anawakilisha utumishi wake kwa kuzingatia maadili kuanzia muonekano yaani mavazi sambamba na matumizi ya lugha sahihi kwenye utoaji huduma.
Aidha Mwl Chembe amesema ni vyema watumishi kuwa makini wakati wa utatuzi wa migogoro ikiwa ni pamoja na kufahamu historia ya mgogoro hiyo ili kuepuka kutengeneza migogoro itokanayo na utatuzi.
kikao cha ushauri Wilaya Arumeru (DCC) kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, wajumbe wake wakiwa ni wenyeviti wa Halmashauri ya Meru na Arusha Vijijini, wenyeviti wa vyama vya siasa Halmashauri ya Meru na Arusha Vijijini, Wakurugenzi wa Halamshauri ya Meru na Arusha Vijijini, wakuu wa Idara na Vitengo wa Halamshauri ya Meru na Arusha Vijijin, Makatibu Tarafa na Watendaji wa kata na Kiiji toka Halmashauri Mbili .
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Arumeru ina Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Halmashauri ya Arusha vijijini.
Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Chembe akizungumza wakati wa kikao cha ushauri cha Wilaya hiyo( DDC).
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Makatibu Tarafa wa Halmashauri ya Meru wakati wa kikao cha DCC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa