Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)wameanza Ziara leo mkoani Arusha kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Arusha na Longido.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Denis L. Londo (MB), wamewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda Katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wajumbe wa Kamati hiyo wamepokea taarifa kutoka kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri hizo na kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa .
Kati ya Miradi inayotembelewa na kamati ni pamoja na mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, Kichomea taka pamoja na ukarabati wa majengo ya zamani katika Hospitali ya Wilaya ya Meru iliyopo Kata ya Akheri.